Saturday 21 March 2015

Barcelona, Real Madrid kufa au kupona Jumapili



Gerard Pique wa Barcelona (kulia) akimiliki mpira katika moja ya mechi za La Liga.

MADRID, Hispania
BEKI wa Barcelona Gerard Pique anasema kila upande una nafasi sawa ya kushinda pambano la Jumapili la Clasico dhidi ya wapinzani wadogo Real Madrid.

Klabu hiyo ya Catalan iko pointi moja mbele ya Real Madrid kileleni mwa Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga.

"Kila upande una nafasi ya asilimia 50 ya kushinda. Wana Cristiano Ronaldo na Gareth Bale, wachezaji wawili wenye nguvu sana, kasi kubwa, hatari sana na wanafunga mabao."

Real Madrid ilishinda mechi mbili za mwisho za Clasicos, na inaweza kuwa mara tatu mfululizo kwa mara ya tatu tangu mwaka 1978.

Hatahivyo, Barcelona haijawahi kupoteza mchezo kwenye uwanja wake wa nyumbani tangu ilipoingi katika ligi mwaka 1929-30.

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi alifunga mabao 17 katika La Liga mwaka 2015, ikiwa ni zaidi ya wachezaji watatu wa Real Madrid Gareth Bale, Karim Benzema na Cristiano Ronaldo combined. Wamefunga mabao matano tu kila mmoja.

Pique aliendelea: "Huu ni moja kati ya mchezo maalum wa mwaka, kwa sababu upinzani kati yetu na tunacheza kama kawaida dhidi yao.

Timu nyingine kubwa, yenye wachezaji wakubwa na hilo ndilo linafanya kuwa maalum zaidi."

Barca imeshinda mara tisa kati ya mechi 10 za mwisho za La Liga na Pique alisema: "Unajihisi una nguvu zaidi na kujiamini.

"Kushinda mechi ya Clasico kutakuwa ni kupiga hatua kubwa mbele. Kuna mechi 10 zimebaki na tumekaribiana sana."

Mshambuliaji wa Real Madrid Benzema alisema: "Tunajua mchezo utakuwa na presha kubwa, lakini hilo ni kawaida kwa kuwa ni mechi kubwa.

"Kila mchezaji anayependa soka anataka kucheza mchezo huo. Endapo tutazuia vizuri tutapata matokeo mazuri.

"Tunaweza kurudia matokeo ya kushinda 3-1 katika mchezo wa kwanza. Tuko katika hali nzuri kushinda na kucheza vizuri kama tulivyocheza awali.

"Kufunga tena kama tulivyofanya katika mchezo ule wa kwanza wa msimu, kiasi fulani kunahitaji bahati na wala hakuna jambo jingine."

No comments:

Post a Comment