*Inacheza na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa
*Simba wageni wa Mgambo JKT Mkwakwani Tanga
Kikosi cha Yanga. |
Na
Mwandishi Wetu
VIGOGO vya soka nchini vya Yanga na Simba leo vitashuka
katika viwanja tofauti kucheza mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika
mashindano ya Afrika, leo watashuka kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
wakiikaribisha Kagera Sugar ya Bukoba.
Wakati Yanga wakiwa Uwanja wa Taifa, wenzao Simba
watakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kuumana na Mgambo JKT
ya huko.
Katika mchezo wa raundi ya kwanza uliofanyika kwenye
uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Yanga walipokea kichapo cha bao 1-0 na hivyo
leo itakuwa na hasira ya kulipa kisasi.
Yanga ambayo ilicheza mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya
Simba kwenye uwanja huo huo na kupokea kichapo cha bao 1-0, na hivyo itataka
kurejea kwa kishindo katika ligi hiyo na kurejea kileleni.
Yanga inahitaji kushinda mchezo wa leo kama inataka
kurudi na kuwa kinara katika msimamo wa ligi.
Azam FC imewashusha Yanga kileleni baada ya kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 na kushika usukani wa ligi hiyo, lakini Yanga leo inaweza
kurejea.
Katika mchezo mwingine leo; Mbeya City ambayo msimu huu
haifanyi vizuri itaikaribisha Stand United ya Shinyanga katika mchezo
utakaopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya.
Msimamo:
MP W D L GF GA +/- Pts
1.Azam 17 9 6 2 24 12 12 33
2.Yanga 16 9 4 3 21 9 12 31
3.Simba 18 7 8 3 22 12 10 29
4.Kagera 18 6 7 5 15 15 0 25
5.Coastal 18 5 8 5 13 12 1 23
6.Mtibwa 18 5 8 5 18 18 0 23
7.JKT Ruvu 18 6 5 7 15 16 -1 23
8.Shooting 18 5 7 6 12 14 -2 22
9.Ndanda 19 6 4 9 17 23 -6 22
10.Stand 18 5 6 7 16 21 -5 21
11.Mgambo 17 6 3 8 11 17 -6 21
12.Polisi 19 4 8 7 13 17 -4 20
13.Mbeya City18 4 8 6 12 16 -4 20
14.Prisons 18 2 10 6 13 20 -7 16
No comments:
Post a Comment