Arsene Wenger. |
LONDON, England
KOCHA Arsene Wenger amesisitiza kuwa hakuna mgogoro wa soka la
England Ulaya licha ya mwaka wa pili mfululizo kwa timu za nchi hiyo kutolewa katika
hatua ya 16 bora katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa, lakini anaamini kua
wakati umefika wa kubadili mfumo wa sheria ya bao la ugenini.
.
Arsenal na Chelsea zote zilitolewa katika mashindano ya Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya kwa faida ya bao la ugenini katika hatua ya kwanza ya mtoano,
zikifungwa na Monaco na Paris Saint-Germain.
Hatahivyo, Wenger, amekuwa kwa muda mrefu akipigania kubadilishwa
kwa sheria hiyo.
'Hiyo ni sheria iliyopitwa na wakati na sasa wakati umefika wa
kuibadilisha, ' alisema kocha huyo wa Arsenal. 'Labda sheria hiyo ituike baada
ya kuchezwa muda wa nyongeza. Ilianzishwa miaka 1960 ili kuziwezesha timu kushambulia zikicheza
ugenini.
'Tangu wakati huo ilipoanzishwa sheria hiyo soka limebadilika sana
na uzito wa bao la ugenini kwa sasa ni mkubwa sana. Labda bao hilo lihesabike
baada ya muda wa nyongeza kama vile katika Kombe la Ligi England.
'Nafikiri kiwango cha Ligi Kuu ya England ni kikubwa na siko
katika hali ya kuelezea sana nini tatizo la soka la Uingereza. Sifiiri kama
kuna tatizo kubwa. '
Wenger sasa anatakiwa kuwaweka tayari wachezaji wake kwa ajili ya
mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Newcastle United wakati
mpambano wa kusaka nafasi nne za kwanza ukiendelea katika ligi hiyo.
Aliongeza: 'hali iko chini ya tumekatishwa tamaa. Mpambano ulidumu
kwa takribani dakika 180 na hatukuwa na tahadhari ya kutosha katika dakika 90
za kwanza. Tunajua kwanini tumetolewa, ni tatizo ka kuzuia katika mchezo wa
kwanza.
SHERIA YA GOLI LA UGENINI:
Endapo mpira utamalizika watimu hizo zikilingana magoli, timu
iliyofunga mabao mengi ugenini itatangazwa kuwa mshindi wa mchezo huo.
Mfano, Monaco iliifunga Arsenal 3-1 ugenini kabla ya kufungwa 2-0
huko Monte Carlo.
Huku matokeo yakiwa bao 3-3, Monaco imesonga mbele baada ya
kufunga goli nyingi zaidi ugenini ukilinganisha na bao mbili za Arsenal
ugenini.
No comments:
Post a Comment