Thursday 12 March 2015

Mawe, reki vyatumika kuwapa mafunzo ya vitendo walimu


Uhaba wa vifaa noma! Mwinga Mwanjala akitumia leki kama mkuki wakati wa kuwafundisha walimu (hawapo pichani) jinsi ya kurusha mkuki wakati wa mafunzo hayo.

Mwanariadha wazamani wa kimataifa wa Tanzania Mwinga Mwanjala akiwaonesha walimu kwa vitendo mchezo kurusha tufe unavyochezwa wakati wa mafunzo katika shule ya msingi Ali hassan Mwinyi Magomeni leo Alhamisi.

Na Cosmas Mlekani
UKISTAAJABU ya Mussa autayaona ya filauni!
Usemi huo umedhirika mapema leo mchana wakati baadhi ya walimu wa shule za msingi mkoa wa Dar es Salaam walipokuwa wakipewa mafunzo ya mchezo wa riadha waliporusha mawe badala ya tufe
.
Mafunzo haya ambayo yalishirikisha zaidi ya walimu 40 wa shule mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam ambapo mbali na riadha pia yalishirikisha michezo mingine kama mpira wa mikono, netiboli, wavu na soka.

Hatahivyo, kihoja hicho kilikuwa kwa walimu kama sita waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya riadha, ambapo kasheshe iliibuka pale walipoanza kufundishwa mazoezi ya vitendo kwenye uwanja wa shule ya Msingi ya Ali Hassan Mwinyi Magomeni.

Mafunzo hayo yalikuwa kuwaandaa walimu kwa ajili ya Michezo ya Shule za MsingiTanzania ya Umitashumta itakayofanyika baadae mwaka huu.
Katika mchezo wa riadha mwanariadha wa kimataifa wa zamani wa Tanzania Mwinga Mwanjala ilimbidi kutumia mawe kuwaonesha waliu hao tufe lilivyo na linavyorushwa.

Mbali na kihoja hicho cha tufe pia ajabu jingine lilitokea wakati walimu wakioneshwa jinsi ya kutupa mkuki, ambapo badala ya kutumika kifaa hicho, badala ya ilitumika leki ya chuma ya kutolea uchafu, ambayo ilionekana wazi kuwapoteza mwelekeo walimu hao kutokana na uzito wa leki hiyo ya chuma.

Mafunzo hayo ya siku tano ambayo yanamalizika Ijumaa, mbali na Mwanjala katika riadha mkufunzi mwingine alikuwa Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui.
Mwinga Mwanjala akiwaonesha walimu jinsi ya kurusha tufe akitumia jiwe kutokana na uhaba wa vifaa.
Washiriki wa semina ambao ni walimu wakiwa katika mafunzo ya vitendo ya kutupa tufe.
Mwanariadha wa kimataifa wa zamani wa Tanzania Mwinga Mwanjala (kushoto) akimuonesha mwalimu Amina Hamisi Ally wa shule ya msingi Ali Hassan Mwinyi jinsi ya kushika kisahani na kukirusha wakati wa mafunzo yaliyofanyika leo Magomeni jijini Dar es Salaam.

Kocha wa mpira wa mikono Clavery Msakuzi (kulia0 akitoa mafunzo kwa baadhi ya walimu wa shule za msingi kuhusu mchezo huo katika mafunzo yaliyofanyika katika shule ya msingi Ali hassan Mwinyi Magomeni Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment