Friday 6 March 2015

Wanne wauawa kwa riasasi, bomu wakijirusha



BAMAKO,Mali
WATU wanne wameuawa kwa mashine gani na bomu la kutupwa kwa mkono katika uvamizi uliofanywa katika klabu moja ya usiku jijini hapa.

Taarifa zilizopatikana hapa zinasema kuwa raia wa Ufaransa alikufa katika baa hiyo ya klabu ya usiku na baadae wawili wengine raia wa Mali waliuawa wakati muuaji akitoweka katika eneo la tukio.

Mtu wa nne aliyeuawa, inasadikiwa I raia wa Ubelgiji,alikufa baada ya bomu kutupwa katika gari lake karibu na mtaa wa jirani.

Watu walioshuhudia tukio hilo walisema watu wanne walikimbia huku wakipiga kelele kwa lugha ya kiarabu "Mungu ni Mkubwa " ("Allahu Akbar").

Ofisa Usalama mwandamizi alisema kuwa watu wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Taarifa hizo zilisema kuwa askari wa Ufaransa waliwasili haraka eneo hilo la tukio baada ya uvamizi huo Jumamosi.

Inaelezwa kuwa askari hao wa Ufaransa walithibitishakuwa mtu mmoja aliyeuawa katika baa alikuwa na uraia wa Ufaransa.

Inaaminika kuwa majeruhi mmoja raia wa Mali ni ofisa polisi, huku mwingine alikuwa ni mlinzi.

Shuhuda huyo alisema kuwa aliwaona watu wanne wakitoroka katika eneo hilo wakiwa na gari huku mwingine akiwa katika bodaboda.

Majeshi ya Kiislamu yamekuwa yakipigana na jeshi la Serikali ya Mali kwa miaka kadhaa sasa.

No comments:

Post a Comment