TIMU ya taifa ya riadha ta Tanzania iliyoshiriki mbio za dunia za
nyika zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Guiyang nchini China, imewasili
salama jijini Dar es Salaam.
Tanzania ilishika nafasi ya sita katika mbio hizo kubwa duniani na
hayo yakiwa ni matokeo mazuri zaidi kuwahi kupata kwa timu ya Tanzania.
Mwanariadha Ismail Juma ndiye aliyeitoa nchi kimasomaso baada ya
kumaliza katika nafasi ya tifa huku wenzake wengine wanne wakishindwa kuwemo
katika 20 bora.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanariadha hao walisema mbio
zilikuwa ngumu lakini walijitahidi na wanafurahia matokeo hayo.
Juma aliyeondoka na kitita cha dola za Marekani 3,000 baada ya
kushika nafasi ya sita, alisema mbio zilikuwa ngumu lakini alijitahidi na
kumaliza katika nafasi hiyo.
Naye kocha wa timu hiyo Francis John alisema kwenye Uwanja wa
Kimataifa wa Ndege wa JK. Nyerere kuwa, vijana wake walijitahidi sana na
kusisitiza kuwa siri ya mafanikio ni kambi waliyopiga huko Mbulu.
Alisema kuwa timu hiyo ilipiga kambi kwa wiki mbili tu huko Mbulu
na kama wangekaa zaidi bila shaka matokeo yangekuwa mazuri zaidi na aliwataka
Riadha Tanzania (RT) kuanza kambi mapema kwa ajili ya kushiriki mashindano
mbalimbali.
Wanariadha wengine wa Tanzania walioshiriki mbio hizo mbali na Ismail Juma aliyemaliza wa sita ni pamoja na
Alphonce Felix, Bazil John, Joseph Teophil na Fabian Nelson, ambao
walishiriki mbio za kilometa 12.
Hatahivyo, wakati wanariadha waliwasili Jumatatu jioni kwa ndege ya Emirates, Nelson hakuwemo na alitarajia angewasili mapema na ndege ya Qatar lakini ndege hiyo ilitua yeye hakuwemo na hakukuwa na taarifa zozote za kutowasili kwake.
No comments:
Post a Comment