Lionel Messi (kulia) akipongezana na Luis Suerez. |
BARCELONA, Hispania
NYOTA Lionel Messi amefunga hat-trick yake
ya 24 katika Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga wakati Barcelona ikitinga kileleni
mwa msimamo wa ligi hiyo.
Barca ilitumia vizuri nafasi ya Real Madrid
kufungwa na Athletic Bilbao wakati Luis Suarez pia akizifumania nyavu mara
mbili wakati timu hiyo ikiibuka na ushindi wa bao 6-1 dhidi ya Rayo Vallecano.
Suarez aliifungia timu yake bao la kuongoza
na Gerard Pique akipachika la pili kabla ya Messi hajafunga la tatu katika
dakika ya 12 ya mchezo huo.
Mara mbili alifunga kwa penati, ambapo
alifunga la nne kabla hajapachika la tano na Suarez alifunga tena.
Timu zote mbili zilijikuta zikimaliza mchezo
zikiwa na wachezaji 10 wakati Román Triguero alipooneshwa kadi ya pili ya njano
kwa kumuangusha Suarez, na kusababisha penati iliyomuwezesha Messi kufanya
matokeo kuwa 3-0.
Barca nao walijikuta wakipata pigo baada ya
beki wao Dani Alves kutolewa nje baada ya kumchezea vibaya Bueno wakati
akielekea langoni na Rayo alifunga penati hiyo na kumfanya kuwa na mabo 13
katika La Liga.
Messi sasa ana mabao 30 ya ligi, ikiwa ni
sawa na mshabuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, ambaye hat-trick zake 23
katika La Liga zimezidiwa na Messi mara moja.
Mess ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa
Argentina mwenye umri wa miaka 27 , sasa anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji
aliyefunga hat-trick nyingi zaidi katika soka la Hispania.
No comments:
Post a Comment