CALIFORNIA, Marekani
BINGWA namba moja katika mchezo wa tenisi duniani kwa
upande wa akina dada Serena Williams (pichani), ametinga hatua ya 16 bora katika
mashindano ya Indian Wells baada ya kuibuka na ushindi wa 6-2 6-0 dhidi ya Zarina
Diyas wa Kazakhstan.
Kwa ushindi huo, Williams sasa atakutana na Mmarekani
mwenzake Sloane Stephens baada ya dakika 53 za raundi ya tatu ya mchezo wa
mashindano ya BNP Paribas Open.
Williams, ambaye aligomea kushiriki mashindano hayo kwa
miaka 14 baada ya kuzomewa mwaka 2001, anasema sasa anajisikia vizuri kucheza
katika mashindano hayo ya California.
"Sasa najisikia kurejea katika hali yangu ya
kwaida hapa," alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33.
"Niliweza kupumzika kwa sababu niliweza kufanya
mengi kwa usahihi na sikufanya makosa mengi kama nilivyofanya katika mchezo
wangu wa raundi iliyopita,"
Stephens beat alimfunga bingwa mara mbili Svetlana
Kuznetsova 7-6 (7-4) 1-6 6-4 na kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ambayo
atakutana na Williams.
Kwa upande wa wanaume, Mswisi Roger Federer alimchakaza
Diego Schwartzman 6-4 6-2 katika raundi ya pili ya mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment