*Hana uhakika wa chakula na kulala kwake ni bustanini
Jimmy Thoronka. |
LONDON, England
MKIMBIAJI wa mbio
fupi kutoka Sierra Leone aliyeingia mitini baada ya kumalizika kwa Michezo ya
Jumuiya ya Madola huko Glasgow, amekuwa akiishia kwa kutangatanga jijini hapa.
Jimmy Thoronka,
20, ambaye ni miongoni mwa wakimbiaji 100 bora nchini mwake lakini hakurejea
nchini huko mwaka jana akidai kuwa alikuwa akihofia ugonjwa hatari wa Ebola.
Thoronka asiye na
makazi anasema kuwa Ebola imeua ndugu zake wa karibu huko Sierra Leone.
"Wakati
mwingine sipaji kabisa chakula. Naosha vyoo vya jumuiya na kulala katika
bustani," aliliambia the Guardian.
Thoronka aliwasili
Glasgow na wachezaji wenzake Julai 2014 wakati ugonjwa wa Ebola ukiwaumefumuka
nchini kwao huku nchi hiyo ikitangazwa kuwa sehemu ya karantini ya ugonjwa huo.
Vifo vilivyosababishwa
na ugonjwa huo nchini Sierra Leone hadi sasa ni zaidi ya 3,500.
Hadi wachezaji 30
wa nchi hiyo walitaka kuongeza viza yao kutoka Septemba mwaka jana ili waweze
kuendelea kukaa Uingereza.
Thoronka, alielezewa
na Chama cha Riadha cha Sierra Leone kama "mkimbiaji wa aina yake, mwenye
uwezo na kasi ya ajabu ", aliyeshindana katika mbio za kupokezana vijiti
ya mita 4x100 katika michezo hiyo, lakini alishindwa kutwaa medali yoyote.
Aliweka muda wake
bora wa sekunde 10.58 katika mbio za mita 100 kabla ya mashindano hayo.
Katika mahojiano,
Thoronka alidai kuwa: Aliambiwa wakati wa michezo hiyo kuwa
mjomba wake aliufa "huenda kutokana na Ebola " na "hakuweza
kumnyamazisha kulia."
Hati yake ya kusafiria iliibwa Glasgow hivyo
anaishi na rafiki yake huko Leicester.
Thoronka alishinda
medali katika mashindano ya Afrika na alitwaa tuzo ya mwanamichezo bora wa
Sierra Leone wa mwaka 2013 inayotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo.
Ndiye alikuwa
mchezaji wa kwanza kutoka Sierra Leone kubeba Kifimbo cha Malkia na kikimbia
nacho katika Michezo ya Jumuiya ya Madola.
No comments:
Post a Comment