DAKAR, Senegal
SENEGAL itakutana na Nigeria katika fainali ya Vijana
2015 baada ya kuifunga Mali 2-1 na kushinda katika mchezo wa nusu fainali ya
pili Alhamisi.
Wenyeji walitinga nusu fainali kama washindi wa pili
katika Kundi A lakini hiyo haikujalisha baada ya kukutana na Mali ambao ni
washindi wa kwanza wa Kundi B.
Ulikuwa mchezo wa kuvutia sana wakati timu hizo mbili
zilipochuana vikali huku Moussa Kone akifunga bao la kuongoza mwanzoni kabisa
mwa mchezo. Bao hilo liliwapa nguvu wenyeji Senegal ikiwa ni kama sekunde 57 tu
tangu kuanza kwa mchezo huo.
Kipa wa Mali Sory Ibrahim Traore hakuweza kulizuia
shuti hilo na mpira kumkuta Kone na kufunga bao la kwanza kati ya mawili.
Hatahivyo, Mali walijibu mapigo haraka na dakika moja
baadae walifanikiwa kusawazisha na kufanya timu hizo kuwa sare kwa bao la mpira
wa mbali lililofungwa na
Alhassane Diallo huko Ibrahima Sy, akiwa katika goli la
Senegal asijue la kufanya.
Senegal, ambayo haijawahi kufuzu kwa mashindano ya Fifa
ya wachezaji wenye umri chini ya miama 20, iliendelea kuweka shinikizo, lakini
Mali ndio nusura wapate bao katika dakika ya 36 kupitia kwa Saliou Guindo.
Kipindi cha pili kilishuhudia timu zote zikifanya
mashambulizi kwa zamu wakati shuti la Mohamed Guilavogui lilipookolewa na Sy, baada
ya kufanya kazi nzuri.
Senegal ilipata bao la ushindi katika dakika 80
lililofungwa tena na Kone na kuiwezesha timu hiyo kutinga fainali hiyo ya
Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chiniya miaka 20.
No comments:
Post a Comment