Monday 23 March 2015

David Cameron atangaza kutoongoza tena



LONDON, England
WAZIRI Mkuu wa Uingereza David Cameron (pichani),amesema kuwa hataongoza kwa kipindi cha tatu katika nafasi hiyo endapo chama chake cha Conservatives kitaendelea kuongoza serikali baada ya uchaguzi mkuu.

Waziri mkuu huyo alisema ikiwa atachaguliwa tena ataongoza kipindi chote cha miaka mitano ya Bunge na baadae ataondoka katika ofisi hiyo inayojulikana sana kama namba 10.

Bwana Cameron alimdokeza katibu wa mambo ya ndani Theresa May, kansela George Osborne na Meya wa jiji la London Mayor Boris Johnson kama watu muhimu awanaoweza kumrithi waziri mkuu huyo.

Chama cha Labour kimekuwa kikimtupia lawama kwa mambo mbalimbali.
Katika mahojiano yake na vyombo vya habari, bwana Cameron alielezea wazito hao katika chama cha Conservative kama "watu muhimu" na "wenye vipaji vya hali ya juu".

Ilielezwa kuwa maoni hayo ya Waziri Mkuu ni sawa na kufanya kampeni.

"Sio tu kutakuwa kumeanzisha kama kampeni katika mbio hizo za uongozi, pia hilo litakuwa limetuma ujumbe kwa wapiga kura kuwa iki wanamuunga mkono waziri mkuu sasa, basi wamemchague yule atakayesimamishwa naye.

No comments:

Post a Comment