PORTO,Ureno
KLABU ya Porto kwa
mara ya kwanza imefuzu kucheza hatua ya nane bora (robo fainali) ya Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya tangu mwaka 2009 baada ya kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Basel.
Kikosi hicho cha
Wareno hakikuwa na mfungaji wake wa mabao mengi Jackson Martinez, lakini
walifanikiwa kuzifumania nyavu mara nne wakati Yacine Brahimi akifunga kwa bao
la mpira wa adhabu la umbali wa mita 20.
Hector Herrera aliongeza
ushindi wa timu yake kabla Casemiro hajafunga tena kwa mpira wa adhabu.
Baadae Vincent
Aboubakar aliongeza la nne kabla Walter Samuel hajapata kadi nyekundu wakati Porto
ikiongeza rekodi yake ya kutofungwa katika mashindano haya hadikufikia mechi
10.
Porto ambao ni
mabingwa wa Ligi ya Mabingwa mwaka 2004 walipata misukosuko kidogo kutoka kwa
timu hiyo ya Uswisi, ambayo ilifuzu kutoka katika hatua ya makundi badala ya
Liverpool.
Na ingawa timu
nyingi za Ulaya zitaona kama Porto ni timu nzuri ya kukutana nayo katika robo
fainali, timu hiyo imeimarika zaidi ikiwa chini ya kocha Muhispania Julen
Lopetegui.
No comments:
Post a Comment