Thursday, 5 March 2015

Wachezaji Nigeria wajeruhiwa kwa risasi


Kikosi cha Kano-Pillars ya Nigeria.

ABUJA, Nigeria
WACHEZAJI watano wa timu ya Kano Pillars wamejeruhiwa kwa risasi na watu wenye silaha katika shambulio lililofanywa na kundi la watu wakati wakisarifi kwenda Owerri kwa ajili ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Nigeria.

"Wachezaji watano waliojeruhiwa kutokana risasi hizo ni pamoja na Gambo, Ogbonaya, Eneji Otekpa, Murtala Adamu, na Moses Ekpai," klabu hiyo iliandika katika mtandao wa Twitter. 

"Watu hao wenye silaha pia walichukua simu za mkononi na vitu vingine vya thamani kutoka kwa wachezaji ".

Kutokana na tukio hilo la uvamizi, mchezo wa Jumamosi dhidi ya Heartland ameahirishwa kwa muda usiojulikana.

Timu ya Kano ilikuwa ikisafiri kwa basi ikiwa na watu 25, wakiwemo wachezaji 18, wakati tukio hilo likitokea saa 7:15 mchana kwa saa za hapa.

Wachezaji watano waliojeruhiwa walipata matibabu katika hospitali ya rufaa ya Centre huko Lokoja.

Kano walikuwa wakijianda kutetea taji la Nigeria, ambapo walianza msimu kwa ushindi dhidi ya Al Malakia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika raundi ya awali wikiendi iliyopita.

Hatahivyo, bado haijajulikana kama ratiba ya mabingwa Kano dhidi ya Moghreb Athletic Tetouane Machi 13 itaendelea kama ilivyopangwa.

No comments:

Post a Comment