Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi |
Na
Mwandishi Wetu, Dodoma
WATUMISHI
zaidi ya 1,000 kutoka Wizara na Idara za Serikali leo watashiriki kwenye
Bonanza la Michezo litakaloongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa
Umma ambaye pia ni Mlezi wa Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za
Serikali (SHIMIWI), litakalofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa SHIMIWI, Daniel Mwalusamba amesema bonanza hilo litatanguliwa na mbio fupi
fupi (jogging) zitakazoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri hadi maeneo ya Bunge na
kurudi kiwanja cha Jamhuri, ambapo mbali na Katibu Mkuu Kiongozi, pia
watashiriki Watendaji Wakuu wa kutoka taasisi mbalimbali za Umma.
Mwalusamba
amesema baada ya mbio hizo wachezaji wote walioshiriki ;watafanya mazoezi ya
viungo na baadaye kushiriki kwenye michezo ya netiboli, soka na kuvuta Kamba.
“Hili
bonanza ni moja ya njia ya kuwaweka watumishi wa umma katika afya njema na
kuepuka magonjwa nyemelezi, ambapo mtumishi ataweza kufanya kazi kwa weledi na
bidi kwa kuwa wanakuwa na afya nzuri,” amesema Mwalusamba.
Pia
amesema bonanza hilo litaendelea kesho (Jumapili) kwa michezo mbalimbali.
Akizungumzia
uwepo wa mashindano ya michezo ya SHIMIWI, ambayo imekuwa ikiahirishwa mara kwa
mara kutokana na sababu mbalimbali, Mwalusamba amesema mashindano hayo yapo na
hayajafutwa na yatafanyika kulingana na taratibu.
“Hii
michezo haijafutwa lakini kumekuwa na mabadiliko ya kiutaratibu, ambapo sasa
serikali yetu ipo katika harakati za ujenzi wa viwanda na sisi ni watu muhimu
wa kuimiza hilo, hivyo michezo itaendelea kama ilivyopangwa,” amesema
Mwalusamba.
Hatahivyo,
amehimiza Watumishi wa Umma kuhakikisha wanatekeleza agizo la Makamu wa Rais,
Mhe. Samia Suluhu Hassan la watumishi wafanye mazoezi kila Jumamosi ya Pili ya kila
mwezi, ili waweze kujiweka vyema katika afya.
Klabu
mbalimbali zimekuwa zikiendesha michezo mbalimbali kwa kushirikisha klabu kwa kushirikiana.
No comments:
Post a Comment