Ronaldo akipiga mpira juu uliompita kipa wa Schalke Timon Wellenreuther na kujaa wavuni. |
MADRID, Hispania
NYOTA wa Real
Madrid Cristiano Ronaldo amefunga mabao mengi katika mashindano ya Ulaya zaidi
ya mchezaji yeyote baada ya kuiwezesha timu yake hiyo kutinga robo fainali ya
Ligi ya Mabingwa baada ya kuiondosha Schalke.
Ronaldo alifunga
mara mbili na kupachika nao lake la 77 na lile la 78 katika mashindano ya
Ulaya, na kumuwezesha kuwa juu ya mchezaji mwenzake wazamani wa Real Madrid Raul
na Lionel Messi wa Barcelona.
Mchezaji huyo wa
kimataifa wa Ureno pia analingana na Messi kwa kushikilia pamoja rekodi ya kuwa
wafunga wa mabao mengi kwa muda wote baada ya kila mmoja kufunga mabao 75 katika
mashindano makubwa ya Ulaya.
WAFUNGAJI BORA ULAYA (IKIWEMO UEFA SUPER
CUP)
78: Cristiano Ronaldo
(Sporting Lisbon, Manchester United, Real Madrid)
77: Raul (Real
Madrid, Schalke)
76: Lionel Messi
(Barcelona)
70: Filippo Inzaghi
(Parma, Juventus, AC Milan)
67: Andriy Shevchenko
(Dynamo Kyiv, AC Milan, Chelsea)
62: Gerd Muller
(Bayern Munich)
62: Ruud van
Nistelrooy (Heerenveen, PSV Eindhoven, Manchester United, Real Madrid, Hamburger)
59: Thierry Henry
(Monaco, Arsenal, Barcelona)
59: Henrik Larsson
(Feyenoord, Celtic, Barcelona, Helsingborgs)
56: Eusebio (Benfica)
Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 30 hakuishia hapo wakati Jumanne usiku alipovunja rekodi
kwa kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Real Madrid kufunga mabao 40 au
zaidi katika misimu mitano mfululizo.
Hatahivyo, winga
huyo wazamani wa Manchester United hakuonekana mwenye furaha sana baada ya
filimbi ya mwisho licha ya timu yao kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya.
Ronaldo alishika
kichwa na hakuwa mtu mwenye furha baada ya timu yake kufungwa 4-3 na kufanikiwa
kusonga mbele kutokana na faida ya bao la ugenini.
Ukweli, Ronaldo alikuwa
mwenye hasira na aliwaambia waandishi wa habari: 'Sitazungumza tena hadi mwisho
wa msimu.'
Mashabiki wa Real
Madrid wakati wote wa mchezo walikuwa wakiwazomea wachezaji wao huku
wakipeperusha vitambaa vyeupe wakionesha kutofurahishwa na kiwango cha timu
yao.
WAFUNGAJI
WANAOONGOZA LIGI YA MABINGWA (UKIONDOA HATUA YA KUFUZU)
75: Cristiano Ronaldo
75: Lionel Messi
71: Raul
56: Ruud van
Nistelrooy
50: Thierry Henry
Mchambuzi wa ITV Roy
Keane alisema hali ya Santiago Bernabeu: ‘Kawaida unapofuzu kwa
robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kunakuwa na shangwe uwanjani lakini
haikuwa hivyo.
'Kila mtu uwanjani
alionekana mwenye kuchanganyiiwa na hakuna aliyeshangilia kufuzu huku kwa robo
fainali.’
Kocha wa Real Madrid
Carlo Ancelotti alikiri wazi baada ya mchezo kuwa, kikosi chake kilistahili
kukosolewa.
‘Ni mbaya kwa sura ya
klabu,’ alisema Ancelotti. ‘Hatua ya mashabiki ni
wazi ilijieleza lakini bado tunatakia kuamka.’
Wakati huohuo,Messi
atakuwa na nafasi ya kukaribia rekodi ya Ronaldo Ulaya wakati Barcelona itakapoikaribisha
Manchester City kwenye uwanja wa Nou Camp Machi 18.
No comments:
Post a Comment