ABUJA, Nigeria
WAANGALIZI wa Kimataifa wameumwagia sifa Uchaguzi Mkuu wa Nigeria,
licha ya matatizo ya kiufundi yalijitokeza, maandamano na taarifa za vurugu baadhi ya maeneo.
Taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki-ilisema
kuwa, sehemu kubwa ya uchaguzi huo ulifanyika kwa amani.
Hatahivyo, upigaji kura uliendelea kwa siku ya pili katika baadhi
ya maeneo nchini Nigeria baada ya kutokea matatizo katika vifaa vya kusoma
vitambulisho vya kupigia kura.
Mchuano mkali unatarajia kuwa kati ya Rais wa sasa Goodluck
Jonathan na mpinzani wake mkubwa Muhammadu Buhari.
Maelfu wa wafuasi wa upinzani huko Rivers State waliandamana
kupinga dhidi ya mauaji ya wafanya kampeni na matatizo yaliyojitokeza katika
upigaji kura.
Tume ya Uchaguzi ya Nigeria ilisema katika taarifa yake kuwa,
kuliwashwa moto huku tume ya uchaguzi ilikuwa ikijaribu kuyafanyia jazu malalamiko hayo.
Bwana Ban aliipongeza Nigeria kufanya uchaguzi huo kwa amani,
licha ya taarifa kuwa uvamizi wa Boko Haram na watu wengine.
Aliwataka wapiga kura kuendeleza hali ya amani wakati wote wa
mchakato huo wa uchaguzi.
Maoni yake yaliungwa mkono na John Kufuor, kiongozi wa Ecowas, ambaye
alisema mchakato mzima wa uchaguzi "ulienda kwa amani… ".
Bwana Jonathan na magavana kama watatu kutoka katika chama tawala
ni miongoni mwa watu chombo vya kusoma alama za vidole kushindwa kusoma
vitambulisho vyao vya kupigia kura.
N
Teknolojia hiyo ilikuwa na lengo la
kupunguza msongamano wa watu na kufanya zoezi kwenda haraka.
No comments:
Post a Comment