*Simba wenyewe kushuka dimbani kesho
Na Mwandishi Wetu
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea tena leo huku vigogo
Yanga wakishuka dimbani kucheza na Mgambo Shooting ya Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani
mjini humo.
Mgambo Shooting hivi karibuni iliitoa nishai Simba kwa
kuichapa 2-0 katika mchezo wa ligi hiyo uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani
mjini Tanga.
Wakati Simba ikilambishwa mchanganya Tanga, wenzao Yanga
waliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar na hivyo kukalia kiti cha
uongozi.
Yanga leo wanakumbana na mkali huyo wa Simba, Mgambo
Shooting kwenye uwanja huo wa Mkwakwani, ambako Simba haikutoka salama.
Yanga iliondoka jijini Dar es Salaam juzi baada ya baada
ya ushindi dhidi ya Kagera Sugar ambao umeifanya iongoze ligi kwa kuwa na
pointi 34 baada ya mechi 17.
Mgambo imekuwa ikizisimbua timu kubwa inapokutana nazo
katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kama Simba, Azam FC na Simba.
Yanga haijawahi kupata ushindi kwenye uwanja huo dhidi
ya
Mgambo Shooting, lakini leo itabidi kupigana kwa nguvu
kuhakikisha inaoondoka na pointi zote tatu ili kuendelea kuwa kileleni.
Kocha wa Mgambo Bakari Shime amesema kuwa Yanga
wajiandae kunyolewa leo na hilo halina ubishi na wasifikiri kama wanaweza
kutoka.
Mgambo Shooting wana pointi 24 katika nafasi yao ya
tano katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 14.
Huko Mtwara; Ndanda FC wataikaribisha JKT Ruvu katika
mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika mchezo wa kwanza JKT Ruvu
ilishinda 2-0.
Nayo Stand United ya Shinyanga itakuwa kwenye uwanja wa
Sokoine mjini Mbeya ikicheza na Kagera Sugar huku Mtibwa
Sugar ambao hawafanyi vizuri sasa watakuwa kwenye uwanaja wa Kambarage
Shinyanga kucheza na Stand United.
Kesho; Simba ya jijini Dar es Salaam itacheza na Ruvu
Shooting wakati Coastal Union itawaalika Azam FC huku
Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji wa Polisi Morogoro
ambayo hivikaribuni ilimtimua kocha wake Rishard Adolf.
Msimamo:
MP W D L GF GA +/- Pts
1.Yanga 17 10 4 3 23 10 13 34
2.Azam 17 9 6 2 24 12 12 33
3.Simba SC 19 7 8 4 22 14 8 29
4.Kagera Sugar 19 6 7 6 16 17 -1 25
5.Coastal
Union 19 5 9 5 14 13 1 24
6.Mgambo JKT 18 7 3 8 13 17 -4 24
7.Mtibwa Sugar 18 5 8 5 18 18 0 23
8.JKT Ruvu 18 6 5 7 15 16 -1 23
9.Mbeya City 19 5 8 6 14 16 -2 23
10.Ruvu
Shooting 19 5 8 6 13 15 -2 23
11.Ndanda 19 6 4 9 17 23 -6 22
12.Stand
United 19 5 6 8 16 23 -7 21
13.Polisi Moro 19 4 8 7 13 17 -4 20
14.Prisons 18 2 10 6 13 20 -7 16
No comments:
Post a Comment