Kikosi cha Dolphins ya Nigeria. |
ABUJA, Nigeria
TIMU ya Nigeria ya Dolphins imetupwa nje ya mashindano ya Kombe la
Shirikisho Afrika.
Kutupwa huko nje kumekuja baada ya Dolphins kushindwa kuwasili kwa
muda uliopnagwa katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya klabu ya Tunisia ya Club
Africain, ambayo sasa imesonga mbele.
Dolphins ilikosa ndege yake kutoka mji wa Port Harcourt kwa sababu
wachezaji wa timu hiyo kutaka kwanza walipwe bonsai zao na kushindwa kuomba
kuahirishwa kwa mchezo huo.
"Kama ubingo wangu ungekuwa sawa na chipu ya komputa basi
wiki hii yote ningeiondoa katika kichwa change," alisema msemaji wa Dolphin
China Acheru.
"Tulitakiwa tumalize kwa wakati matatizo yetu ya ndani. Kama
tungeyashughulikia mapema tusingepata matatizi haya.
"Wachezaji walikuwa wakitaka dola 500 zaidi kwa kila mmoja
kwa safari hiyo. Tulikubali kutoa dola 750 lakini wakati tunalikubali hilo
tayari tulikosa ndege. Mwishoni wachezaji walikubali kubeba lawama kuwa wao
ndio walisababisha kuchelewa ndege na kila moja lipokea dola 600.
"Ni wazi ni upotezaji wa muda na wiki ya kusahau."
Shirikisho la Soka Afrika
(CAF) lilitoa taarifa katika mtandao wa Dolphins "hawakutokea katika
pambano lao huko Rades Jumamosi, Machi 14 mwaka 2015…. ".
Kwa matokeo hayo, "mwamuzi the referee acknowledged
forfeiture of Dolphins".
No comments:
Post a Comment