MADRID, Hispania
RAIS wa Real Madrid Florentino Perez ameitisha mkutano wa dharura
na waandishi wa habari kuelezea kumuunga mkono kocha Carlo Ancelotti na kumtetea
Gareth Bale aliyekalia kuti kavu katika timu hiyo.
Marca, gazeti maarufu la michezo la jijini hapa, lilidai kuwa,
kocha huyo wazamani wa Chelsea alikaribia kutupiwa virago, ulisomeka ukurasa
wake wa mbele, huku ukiwa na kichwa cha habari: 'Hakuna Zaidi'.
Marca ilidai kuwa kipigo cha timu hiyo dhidi ya Barcelona kwenye
uwanja wa Nou Camp ndani ya siku 10 kutashuhudia mwisho wa Ancelotti, aliyeiongoza
timu hiyo kutwaa mataji mawili lile la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na la Mfalme.
Lakini, akionekana kujibu moja kwa moja ripoti ya gazeti hilo,
Perez alisema: 'Taarifa hizo sio za kweli na hazikubaliki kabisa kwa sasa….
Napenda kutoa maelezo kwa mpangilio kuwa klabu ina imani kubwa na
kocha wetu na wachezaji pia. Na ninataka kusema kuwa, nina kanusha vikali
taarifa hizo na siku zijazo na wiki Carlo Ancelotti atabaki kuwa kocha wa Real
Madrid.
'Mimi kama rais wa Real Madrid, nawaomba mashabiki wetu kumuunga
mkono kocha na wachezaji wetu na ninawaomba kujisikia fahari kuwa nao.'
Real haijashinda katika michezo yake mitatu, na kuachia uongozi ea
Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga kwa Barcelona na imefuzu kibahati kwa robo
fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa faida ya bao la ugenini baada ya
kuchapwa 4-3 nyumbani na Schalke Jumanne usiku.
No comments:
Post a Comment