Tuesday, 17 March 2015

Penati zaipeleka Atletico Madrid robo fainali Ulaya


Kipa wa Leverkusen Bernd Leno akiruka bila mafanikio kuzuia penati ya Torres.

MADRID, Hispania
TIMU ya Atletico Madrid imetinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya kuichapa kwa penati Bayer Leverkusen.

Kufuatia kufungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza huko Ujerumani, Atletico ilisawazisha baada ya bao la dakika ya 27 lililowekwa kimiani na Mario Suarez baada ya shuti lake kumbabatiza Omer Toprak.

Wenyeji nusura wapate bao la ushindi katika muda wa nyongeza lakini kipa wa Leverkusen Bernd Leno aliokoa shuti hilo.

Hakan Calhanoglu, Toprak na Stefan Kiessling wote walikosa penati zao kwa Leverkusen wakati Atletico ikiibuka na ushindi wa penati 3-2.

Kipa aliyeingia akitokea benchi Jan Oblak mwaka jana hakuwa na bahati baada ya Atletico kufungwa katika fainali, akichukua nafasi ya Miguel Angel Moya, aliyeumia katikati ya kipindi cha kwanza.

Oblak alishindwa kuwa kipa wa kwanza wa Atletico tangu alipohamia kutoka Benfica kwa ada ya uhamisho ya pauni Milioni 12.6 akichukua nafasi ya Thibaut Courtois, aliyerejea Chelsea baada ya miaka mitatu ya kucheza kwa mkopo.

Lakini kipa huyo Mslovenia mwenye umri wa miaka 22 aliokoa penati ya Calhanoglu baada ya Raul Garcia kuwakosesha wenyeji penati ya kwanza.

No comments:

Post a Comment