Wednesday 18 March 2015

Bolivia yafuta pambano na Nigeria ikihofia usalama



ABUJA, Nigeria
TIMU ya taifa ya Bolivia imefuta mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Nigeria uliopangwa kufanyika Machi 26 huko Uyo kwa sababu za kisalama, imeelezwa.

Rais wa Shirikisho la Soka la Bolovia Carlos Chavez alisema: "Matatizo ya kijeshi na hali mbaya ya kisiasa huko Nigeria ndiko kulikoilazimu nchi hiyo kuufuta mchezo huo."

Hatahivyo, viongozi wa Nigeria wamesema kuwa wamesikitishwa na kitendo hicho kwani kila kitu kilikuwa katika utaratibu mzuri kwa ajili ya pambano hilo.

Hiyo ikiwa na maana kuwa kipa wa Nigeria Vinent Enyeama itambidi kusubiri ili kufikisha mchezo wa 100 wa kuichezea timu hiyo ya taifa.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 alitarajia kufikisha idadi hiyo ya mechi wakati wa mchezo huo na Bolivia, baada ya kutangazwa katika kikosi cha wachezaji 28 wa Super Eagles kilichopo chini ya kocha wa muda Daniel Amokachi.

Sasa itambidi kipa huyo kusubiri hadi kucheza mchezo huo wa 100 hadi pale Nigeria itakapojipima nguvu na Afrika Kusini Jumapili ya Machi 29 labda kama Shirikisho la Soka la Nigeria litatafuta mchezo mwingine badala ya ule wa America ya Kusini.

Mshambuliaji aliye katika fomu wa West Brom, Brown Ideye naye yumo katika kikosi hicho, pamoja na Odion Ighalo wa timu ya daraja la kwanza ya Watford.

Mshambuliaji majeruhi wa Stoke Victor Moses naye pia yuko katika skwadi hiyo ambaye amemuhakiishia kocha Amokachi kuwa atakuwa fiti kucheza mchezo huo.

Kikosi hicho cha timu ya taifa ya Nigeria kitakuwa pamoja na kusafiri kwenda Afrika Kusini kucheza mchezo mwingine wa kirafiki Jumapili, Machi 29.

Kikosi Kamili cha Nigeria:
Makipa: Vincent Enyeama (Lille OSC, Ufaransa); Theophilus Afelokhai (Kano Pillars); Chidiebere Eze (Ifeanyi Ubah United).

Mabeki: Chima Akas (Sharks FC); Godfrey Oboabona (Rizespor FC, Uturuki); Azubuike Egwuekwe (Warri Wolves); Nelson Ogbonnaya (Heartland FC); Kenneth Omeruo (Middlesbrough FC, England); Akeem Latifu (Aalesunds FC, Norway); Leon Balogun (Darmstadt 98, Ujerumani).

Viungo: Ogenyi Onazi (SS Lazio, Italia); Steven Ukoh (Biel-Bienne FC, Uswisi); Sone Aluko (Hull City, England); Hope Akpan (Reading FC, England); John Ogu (Hapoel Be'er Sheva, Israel); Michael Babatunde (Volyn Lutsk, Ukraine); Joseph Nathaniel (Sharks FC); Kingsley Sokari (Enyimba FC).

Washambuliaji: Ahmed Musa (CSKA Moscow, Russia); Aaron Samuel (Guangzhou R&F, China); Brown Ideye (West Brom, England); Odion Ighalo (Watford FC, England); Anthony Ujah (FC Cologne, Ujerumani); Moses Simon (KAA Gent, Ubelgiji); Ubong Moses (Kano Pillars); Stanley Dimgba (Warri Wolves); Mfon Udoh (Enyimba FC); Standby - Victor Moses (Stoke City, England).

No comments:

Post a Comment