Na Mwandishi Wetu
SIMBA jana ilidhihirisha umwamba mbele ya
Yanga baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wao hao wa jadi
katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Bao lililowafanya wapenzi wa Yanga kulala
mapema huku wenzao wa Simba wakichonga sana, lilifungwa na mshambuliaji
wazamani wa Yanga Mganda Emmanuel Okwi (pichani) katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
Ushindi huo wa Simba haukutarajiwa kabisa
na mashabiki na viongozi wa Yanga mabao kwa wiki nzima walionekana kutamba kuwa
timu yao itaibuka na ushindi kwani ina kikosi imara na cha uhakika.
Bao hilo pekee katika mchezo huo lilifungwa
na Okwi katika dakika ya 51 ikiwa ni dakika zaidi, aliupiga mpira kifundi na
kujaza wavuni na kuibua chereko kwa wapenzi wa Simba huku wenzao wa Yanga
wakijipa matumaini kuwa timu yao itarudisha na kupata bao la ushindi.
Tangu awali Simba ilionekana ingeibuka na
ushindi baada ya timu yao ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 kuibuka na
ushindi wa bao 4-2 dhidi ya wenzao wa Yanga katika mchezo uliochezwa mapema.
Katika mchezo huo Haruna Niyonzima
alitolewa uwanjani kwa kadi Nyekundu baada ya kukaidi amri ya mwamuzi Martin
Saanya wa Morogoro, ambapo alipiga mpira langoni licha ya kupigiw filimbi ya
kuotea na kusababisha kuoneshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje.
Vikosi
Vilivyoanza leo:
SIMBA
SC: Ivo Mapunda, Kessy Ramadhan, Mohhamed
Hussein, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Abdi Banda/Simon Sserunkuma, Ramadhani
Singano, Jonas Mkude, Ibrahim Ajib/ Elias Maguli, Said Ndemla na Emanuel Okwi.
YANGA
SC: Ally Mustafa,Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir
Haroub, Kelven Yondani, Said Juma, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amis Tambwe, Mrisho
Ngassa/ Khap Sherman na Danny Mrwanda/ Hussein Javu.
WAAMUZI:
Mwamuzi
wa kati: Martin Saanya kutoka Morogoro.
Mwamuzi
msaidizi namba moja:Soud Lila kutoka Dar es Salaam
Mwamuzi
msaidizi namba mbili:Frolent Zabron wa Dodoma.
Mwamuzi
wa akiba au mezani: Islael Mjuni.
No comments:
Post a Comment