Rais Goodluck Jonathan (kushoto) na
MTAWALA wazamani wa kijeshi Muhammadu Buhari amekuwa mgombea wa
kwanza wa upinzani kushinda uchaguzi mkuu nchini Nigeria.
Chama cha Jenerali Buhari kilisema kuwa, mpinzani wake ambaye
alikuwa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, alikubali matokeo hayo na kumpongeza
mwanajeshi huyo mstaafu.
Wakati akikubali kushindwa, Jonathan alikuwa amepitwa na Buhari karibu
kura milioni mbili.
Waangalizi wa uchaguzi huo waliupongeza lakini kulikuwa na tetesi
za vurugu, zilizosababisha wasiwasi kuwa zingesababisha maandamano na vurugu.
"Rais Jonathan alimpigia simu Jenerali Muhammadu Buhari, mshindi
wa uchaguzi, kumpngeza, “alisema Lai
Mohammed, ambaye ni msemaji wa Chama cha Jenerali cha All Progressives Congress
(APC).
Msemaji alimpongeza Bwana Jonathan, akisema: "Atabaki kuwa
shujaa wan chi hii kwa kitendo chake cha kukubali matokeo…."
"Yeyote atakayejaribu kuleta vurugu kwa madai ya kushindwa
katika uchaguzi atakuwa akifanya hilo kwa faida yake, " aliongeza.
Hiki ni kipindi muhimu kwa historia ya Nigeria. Haijawahi kutokea
rais aliye madarakani kushindwa katika uchaguzi.
No comments:
Post a Comment