Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania, Nicolaus Mihayo (wa pili kulia). |
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Mpira wa Mikono Tanzania (Taha) kwa kushirikiana na
Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kimeandaa kozi ya awali ya kimataifa kwa
ajili ya walimu wa shule sekondari itakayofanyika katika shule ya Filbert Bayi
Kibaha kuanzia Aprili 13 hadi 24 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Taha, Nicolaus Mihayo alisema hivi karibuni kuwa,
kozi hiyo itawashirikisha jumla ya walimu 30 kutoka shule za Tanzania Bara na
Zanzibar.
Akifafanua zaidi alisema kuwa, Tanzania Bara itakuwa na walimu 20
wakati Zanzibar wataleta walimu 10.
Mihayo alisema kuwa kozi hiyo ya ufudishaji wa mpira wa mikono
imewalenga walimu ili baada ya kumaliza waende kuueleze mchezo huo mashuleni
Alisema lengo la Taha sasa kuhakikisha mchezo huo unasambaa
mashuleni na mitaani baada ya muda mrefu kuchezwa na taasisi za kijeshi.
Alisema kuwa kozi hiyo itafundishwa na mkufunzi wa kimataifa
kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono (IHF), Peter Hans
atakayesaidiwa na kocha wa siku nyingi nchini Daid Kiama.
Mihayo alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na ni matumaini
yao wote waliothibitisha kushiriki watakuwepo katika kozi hiyo maalum kwa
walimu wa shule za msingi na sekondari.
No comments:
Post a Comment