LISBON, Ureno
BINGWA mara mbili wa Olimpiki Mo Farah ameshinda mbio
za nusu marathoni za Lisbon na kuweka rekodi ya muda bora kwa Ulaya, na kuwa
Muingereza wa kwanza kukimbia mbio hizo chini ya dakika 60.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 31 alishinda mbio
hizo za maili 13.1 kwa kutumia dakika 59 na sekunde 32, na kuvunja rekodi
iliyowekwa miaka 14 kwa
sekunde 20 na Mhispania Fabian Roncero.
Farah, pia ndiye bingwa wa dunia wa mbio za mita 5,000
na 10,000m, `akimchapa’
Mkenya Micah Kogo.
Rekodi ya dunia ya 58:23 iliwekwa na mwanariadha wa
Eritrea Zersenay Tadese katika mashindano ya mwaka 2010 yaliyofanyika Lisbon.
Mkenya Kogo, mshindi wa medali ya shaba wa mbio za mita
10,000 kutoka katika Olimpiki ya Beijing mwaka 2008, alikuwa mmoja wa watu sita
walishiriki mbio hizo na Farah wakiwa na rekodi ya kukimbi chini ya dakika 60
kwa umbali huo.
Pia kulikuwa na mafanikio kwa Muingereza David Weir aliyeshiriki
katika mbio za `wheelchair’na Shelly Woods ambaye anaendelea kujiandaa
kwa mbio za mwezi ujao za London Marathon.
Weir alimshinda mpinzani wake Mswis Marcel Hug, ambapo
mshindi aliamriwa kwa picha au `photo-finish’ wakati Woods alifanya kweli dhidi ya mpinzani wake
Muingereza Jade Jones.
No comments:
Post a Comment