Wednesday 11 March 2015

Chelsea yafungashwa virago na Paris St-German


Diego Costa akichuana na beki wazamani wa Chelsea David Luiz wakati timuhizo zilipochuana.


LONDON, England
KOCHA wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa wachezaji wake hawakuweza kabisa kubadili akili yao na kucheza na mazingira wakati timu yao ikitolewa katika hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na Paris St-German iliyokuwa na wachezaji 10.

Mabingwa hao wa Ufaransa mara mbili walitoka nyuma katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Stamford Bridge na kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.

"Mchezo wetu haukuwa mzuri kabisa," alisema Mourinho. "Wapinzani wetu walikuwa bora zaidi yetu, waliendana na shinikizo la mchezo.

"Tulijaribu kushinda lakini kipindi wakati wamebaki wachezaji 10 tulihisi shinikizo zaidi."

Aliongeza: "Paris St-Germain walistahili kushinda. Wakati timu haiwezi kuzuia kona mbili na kuruhusu magoli mawili ya kona hatukustahili kushinda."

Wageni walicheza saa moja ya muda wa kawaida na dakika 30 za nyongeza wakiwa bila ya mshambuliaji wake Zlatan Ibrahimovic baada ya mchezaji huyo kutolewa nje baada ya kumchezea vibaya Oscar.


Lakini, kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza huko Paris, bao la kichwa la Thiago Silva limewawezesha kufuzu kwa faida ya bao la ugenini na kufanikiwa kulipa kisasi chamsimu uliopita walipotolewa na Chelsea katika robo fainali.

"Wanasababu ya kushangilia na niliwaambia wachezaji wangu baada ya mchezo nilipiga meza na kiti na milango, lakini ni muda wa kutulia na kuchambua kama timu, alisema Mourinho.

No comments:

Post a Comment