Mmoja wa wafungaji wa mabao ya Yanga ilipocheza na Mgambo Jumamosi Amis Tambwe. |
Na Mwandishi Wetu, Tanga
YANGA ya Dar es Salaam imeendelea kuiwashia indiketa Azam FC
katika mbio za Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wababe wa Simba
Mgambo Shooting kwa bao 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa
Mkwakwani.
Yanga ilipata bao lake la kwa kwanza katika dakika ya 78
kupitia kwa Simon Msuva na kuifanya timu hiyo kujiweka katika nafasi nzuri ya
kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
Mrundi Amis Tambwe ambaye alitemwa na Simba kwa `fitiuna’
aliihakikishia Yanga ushindi baada ya kufunga bao katika dakika ya 87 na
kuiwezesha timu hiyo kuondoka mjini Tanga na pointi zote tatu.
Kwa ushindi huo, Yanga sasa wamefikisha pointi 37 baada ya
kucheza mechi 18 wakifuatiwa na mabingwa watetezi Azam FC ambao wako nyuma kwa
pointi nne na hivyo kuzidi kujikita kleleni.
Tambwe alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha krosi
iliyochongwa na mchezaji mmoja wa Yanga.
Hatahivyo, ushindi huo wa Yanga haukuja kirahisi kwani
Mgambo Shooting nao walifanya mashambulizi kadhaa lakini bahati haikuwa yao.
Mechi za ligi hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 14
itaendelea Jumapili kwa Simba ya jijini Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shooting
wakati Coastal Union itawaalika Azam FC huku Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji
wa Polisi Morogoro ambayo hivi karibuni ilimtimua kocha wake Rishard Adolf.
No comments:
Post a Comment