LONDON, England
CRISTIANO Ronaldo (pichani) ndiye
mwanasoka tajiri zaidi duniani huku akiwa na utajiri wa kiasi cha pauni Milioni
152 ikiwa ni pauni 7 zaidi ya mpinzani wake Lionel Messi.
Baada ya kufanya
vizuri mwaka 2014 na kushuhudia Ronaldo akiiwezesha Real Madrid kupata
mafanikio katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na kushinda tuzo ya Ballon d'Or, aliongeza
tofauti ya nafasi ya utajiri wake na nyota huyo wa Barcelona na Argentina.
Kwa mujibu wa orodha
ya matajiri iliyotolewa na Goal.com Alhamisi, Ronaldo na Messi ndio wanaotamba
kwa utajiri zaidi kuliko wanasoka wengine kwa sasa katika soka la kulipwa.
Jumla ya utajiri
wao, ambao unatokana na matangazo pamoja na mishahara na bonasi, ni zaidi ya
ule alionao Neymar, anayeshika nafasi ya tatu akiwa na utajiri wa thamani ya pauni
Milioni 97.9.
Zlatan Ibrahimovic
wa Paris Saint-Germain na Sweden anautajiri wa Pauni Milioni 76.1,
wakati Wayne Rooney wa Manchester United ndiye anayeongoza kwa utajiri kwa
wachezaji Waingereza akishika nafasi ya tano kwa dola Milioni 74.6.
Kaka wa Brazil
yeye kwa sasa anashikilia nafasi ya sita akiwa na pauni Milioni 69.6,
akifuatia na Samuel Eto'o (pauni Milioni 63.1), Raul (pauni Milioni 61.6) na Ronaldinho (Milioni 60.2).
Kiungo wazamani wa
England Frank Lampard, kwa sasa anaichezea Manchester City kabla yakwenda New
York City katika Ligi Kuu ya Marekani, anakamilisha orodha ya 10 bora kwa kuwa
nba utajiri wenye thamani ya pauni milioni 58.
Wachezaji wengine Waingereza
waliopo katika 20 bora ni Rio Ferdinand (nafasi ya 12, pauni Milioni 52.2),
Steven Gerrard (nafasi ya 14, pauni Milioni 46.4) na John Terry (nafasi ya 20, pauni
Milioni 40.6).
Lionel Messi wa Barcelona. |
Kuna wachezaji
wengine wawili zaidi wa Man City katika orodha hiyo, pamoja na Yaya Toure katika
nafasi ya 15 akiwa na utajiri wa pauni Milioni 44.9 na Sergio
Aguero katika nafasi ya 19 na utajiri wa pauni Milioni 42.
Mwaka jana orodha
ya matajiri wa Goal iliyotolewa ilibainisha kuwa Ronaldo alikuwa na utajiri
wenye thamani ya pauni Milioni 122, huku Messi akimkimfuatia
kwa nyuma kwa utajiri wa pauni Milioni 120.5.
No comments:
Post a Comment