Thursday, 12 March 2015

Tanzania yapanda viwango vya soka kimataifa yawa ya 100



 
Na Mwandishi Wetu
TANZANIA imepanda katika viwango vya soka na kuwa ya 100 kwa ubora, kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa).

Kwa mujibu wa viwango hiyo vilivyotolewa leo, Tanzania imepanda kwa nafasi saba huku Hispania ikitolewa katika 10 bora na Italia ikirejea katika nafasi hizo 10.

Tanzania katika viwango vya Machi imejikusanyia jumla ya pointi 331 wakati viwango vilivyopita ilikuwa na pointi 315 tu.

Ujerumani imeendelea kuongoza baada ya kujikusanyia pointi 1770 wakati viwango vilivyopita ilingoza pia lakini ikiwa na pointi 1729 huku Argentina ikishika nafasi ya pili 1577 Colombia ni ya tatu, Ubelgiji ni ya nne na Uholanzi ni ya tano wakati Brazil iko katika nafasi ya sita, Ureno ni ya saba.

Ufaransa inashikilia nafasi ya nane, Uruguay iko katika nafasi ya tisa na Italia ndi inafunga katika timu zilizopo katika nafasi 10 bora ikiwa imejikisanyia jumla ya pointi 1146.

Hispania imeondolewa katika 10 bora na sasa iko katika nafasi ya 11 baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 1130 wakati mwezi uliopita ilijikusanyia jumla ya pointi 1144.

Katika Afrika Algeria imeendelea kuongoza baada ya kushika nafasi ya 18 baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 989 wakati mwezi uliopita ilipata pointi 981.

No comments:

Post a Comment