Sunday, 22 March 2015

Dick Advocaat aanza kwa mkosi Ligi Kuu England



LONDON, England
KUREJEA kwa Dick Advocaat katika klabu ya Sunderland kumekuwa kwa mkosi baada ya bao la Diafra Sakho kuiwezesha West Ham kuibuka na ushindi wa 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika kwenye uwanja wa Upton Park.

Mholanzi huyo, aliyechukua nafasi ya mtangulizi wake aliyetimuliwa Gus Poyet wiki iliyopita, alijikuta akianza vibaya kibarua hicho kwa kipigo katika Ligi Kuu ya England.

Kikosi hicho kinachojulikana kama Paka Weusi ambacho Adam Johnson alicheza kwa dakika 17 baada ya klabu kumuondolea kifungo kufuatia kukamatwa, wako pointi moja kutoka timu zinazoshika nafasi tatu za mwisho.

Kwa ushindi huo, West Ham imepanda juu ya Stoke katika nafasi ya tisa.

Huo ni ushindi wa pili katika mechi 12 za Ligi Kuu ya England kwa kikosi hicho cha kocha Sam Allardyce, ambacho kilikuwa katika nafasi ya nne wakati wa Krismas.

Vipigo kwa wapinzani wao Burnley, Leicester na Aston Villa mapema jana Jumamosi kuna maana kuwa, kipigo cha timu hii sasa hakina machungu sana kama kilivyokuwa awali, lakini Advocaat, 67, itambindi kufanyia kazi nafasi ilizokosa timu hiyo.

Defoe alikuwa mmoja kati ya washambuliaji watatu waliochaguliwa na makocha watano wa timu hiyo katika kipindi cha miaka sita na nusura aipatie timu yake bao la kuongoza dhidi ya timu ambayo ilikuwa inalingana nayo kwa kiwango.

Hatahivyo, mchezaji huyo wa kimataifa wazamani wa England, alishindwa kutumia vizuri nafasi alizopata.
Guus Hiddink ni kocha pekee kutoka Uholanzi aliyewahikushinda mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Engald.

No comments:

Post a Comment