Sunday 22 March 2015

Coca Cola, Zara Charity kudhamini Ngorongoro Marathoni


Baadhi ya wanariadha wakichuana katika mbio za Ngorongoro Marathoni mwaka jana.

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Coca Cola ndio mdhamini mkuu mpya wa mbio za Ngorongoro Marathoni zitakazofanyika Aprili 18.

Mmoja wa waratibu wa mbio hizo Meta Petro alisema kuwa Coca Cola imeungana na Kampuni ya Zara Charity kudhamini mashindano hayo makubwa ya kila mwaka.

Alisema kuwa awali Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo ndio ilikuwa mdhamini mkuu wa mbio hizo ambazo huanzia katika lango kuu la kuingilia na kutokea katika Bonde la Ngorongoro, lakini mwaka huu Coca Cola ndio watadhamini mbio hizo.

Hatahivyo, Petro hakusema sababu za Tigo kutodhamini tena mbio hizo lakini alisiaitiza kuwa tayari wanariadha kibao nyota wa Tanzania wanaendelea kujiandikisha kwa ajili ya mbio hizo, ambazo kila mwaka zimekuwa zikiongezeka msisimko wake.

Aidha, Petro alisema kuwa waandaaji wameongeza zawadi kwa washindi, ambapo mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume na wanawake, kila mmoja ataondoka na kitita cha Sh. Milioni 1.2, wakati mwaka jana mshindi wa nafasi hiyo alipewa sh. Milioni 1 kwa mwanaume na mwanamke 500,000, mshindi wa pili mwaka huu atapewa sh. 600,000 wakati mwaka jana alipata 500,000 na wanawake alipata 200,000.

Kwa mshindi wa tatu mwaka huu ataondoka na sh. 400,000 wakati mwaka jana mshindi wa nafasi hiyo kwa wanaume alipewa sh.300,000 na kwa wanawake alipewa 200,000.

Alisema kuwa mbio za mwaka huu wanatarajia wanariadha zaidi kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki mbio hizo ambazo hutumika kupiga vita ugonjwa hatari wa malaria na kutangaza utalii wa ndani na nje.

No comments:

Post a Comment