*Azam FC kuikaribisha JKT Ruvu
Kikosi cha Yanga Africans. |
Na Mwandishi Wetu
PATASHIKA nguo
kuchanika kesho wakati watani wa jadi wa Yanga na Simba watakapovaana kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Huo ni mchezo wa
marudiano wa timu hizo baada ya ule wa kwanza uliofanyika katika duru la kwanza
kutoka sare.
Timu hizo
zinachuana wakati Yanga wakiwa kileleni baada ya kujikusanyia pointi 31 huku wenzao
wa Simba wakiwa katika nafasi ya nne baada ya kuwa na pointi 23 baada ya
michezo 16. Yanga wamecheza mechi 15.
Kikosi cha Simba Sports Club. |
Simba wako kambini
Zanzibar na wenzao Yanga wamejichimbia mjini Bagamoyo katika Chuo cha Uvuvi
Mbegani, ambapo timu zote zimetamba kuibuka na ushindi.
Kitakwimu, Yanga
wako vizuri zaidi kwani katika mechi za hivi karibuni wameshinda michezo mingi
ukilinganisha na wenzao wa Simba, ambao ukiondoa mechi dhidi ya Prisons hivi
karibuni, wamekuwa hawafanyi vizuri.
Yanga katika hali
ya kuonesha wako vizuri zaidi, wiki iliyopita walizifunga Tanzania Prisons na
Mbeya City katika mchezo wa ligi hiyo kwenye Uwnja wa Kumbukumhu ya Sokoine
mjini Mbeya.
Mechi zingine
kesho Jumapili ni Mgambo JKT wataikaribisha Ndanda FC na Mtibwa Suga dhidi ya Mbeya
City.
Aidha, ligi hiyo
itaendelea leo katika viwanja tofauti wakati Polisi Moro itakuwa mwenyeji wa Ruvu
Shooting huku Coastal Union ikicheza na Kagera Sugar, JKT Ruvu watatoana jasho
na mabingwa watetezi Azam FC.
Msimamo:
MP W D L GF GA +/- Pts
1Young Africans 15 9 4 2 21 8 13 31
2 Azam FC 15 7 6 2 22 12 10 27
3 Kagera Sugar 17 6 6 5 13 13 0 24
4 Simba SC 16 5 8 3 20 12 8 23
5 Mtibwa Sugar 16 5 7 4 17 16 1 22
6 Coastal Union 17 5 7 5 11 10 1 22
7 Ndanda 17 6 4 7 16 19 -3 22
8 Stand United 17 5 6 6 16 18 -2 21
9 Ruvu Shooting 17 5 6 6 12 14 -2 21
10JKT Ruvu 16 5 5 6 14 15 -1 20
11Polisi Moro 17 4 7 6 13 16 -3 19
12Mbeya City 16 4 6 6 11 15 -4 18
13Mgambo JKT 15 5 2 8 8 16 -8 17
14 Prisons 17 1 10 6 10 20 -10 13
No comments:
Post a Comment