MONACO, Ufaransa
ZIMEBAKI siku chache kabla ya kufanyika kwa mbio za
dunia za nyika zitakazofanyika Guiyang, China Machi 28, mashindano ya mwaka huu
yatashindanisha wanariadha wengi zaidi.
Zaidi ya wanariadha 447 kutoka nchi 51 wanajiandaa
kutua Guiyang kwa ajili ya mbio hizo ikiwa ni idadi zaidi ya wale walioshiriki
mwaka 2013 (wanariadha 400 kutoka nchi 41), 2011 (wanariadha 423 kutoka nchi 51)
na 2010 (wanariadha 437 kutoka nchi 51).
Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF) wiki ijayo
litachapisha orodha, lakini hapa tunaangalia wanariadha 10 ambao watakuwa tishio
katika mbio hizo.
Wakubwa
wanaume:
Bedan Karoki (KEN)
Bingwa huyo wa Kenya anachukuliwa zaidi kama mmoja wa
wanariadha mahiri katika mbio za nyika duniani, lakini Karoki ameshinda mara
mbili mbio hizo.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 24 atashiriki
mbio za dunia za nyika zitakazofanyika Guiyang.
Polat Kemboi Arikan (Uturuki)
Arikan alitawala mbio za nyika za Ulaya Desemba, lakini
katika mbio za Guiyan anatarajia kuwa mmoja wa washindani wakubwa kwa sasa
katika mbio hizo.
Chris Derrick (Marekani)
Mshindi wa timu iliyotwaa medali ya fedha miaka miwili
iliyopita, Derrick ndiye tegemeo la Marekani huko China.
Badaa ya kushinda mbio
za kilometa nane huko Edinburgh
Januari, aliendelea kushinda mbio za taifa za nyika kwa sekunde 30.
Wanawake wakubwa
Emily Chebet (Kenya)
Bingwa mara mbili wa mbio za nyika za dunia na
aliongezwa katika timu ya taifa ya Kenya.
Ding Changqin (China)
Bingwa wa medali mbili katika mbio za uwanjani mwaka
jana katika mashindano ya Asia, Ding
anabeba matumaini ya taifa.
Mwaka jana alishinda mbio fupi na ndefu katika
mashindano ya mbio za nyika ya China kwa tofauti kubwa.
Jacqueline Martin (Hispania)
Ni mwanariadha mwenye umri wa miaka 40 na atashiriki
mashindano hayo kwa mara ya 14, ikiwa ni miaka 23 tangu aanze kushiriki mbio
hizo. Ni wanawake wawili pekee katika historia ya mashindano hayo wenye uzoefu
zaidi ya wanariadha wengine.
No comments:
Post a Comment