Baadhi ya watu, ndugu na wazazi wa wanafunzi wanaofanya mitihani wakiwapa majibu watahiniwa hao katika jimbo moja huko India. |
DEHLI, India
WATU zaidi ya 300 wamekamatwa katika jimbo la Bihar nchini
India wakidaiwa kuwasaidia kuwapa wanafunzi majibu ya mtihani wa taifa ya masomo
mbalimbali.
Watu hao wengi wakiwa ni wazazi na ndugu wa wanafunzi hao,
walipanda ukuta katika majengo ya shule hiyo na kuwapa majibu wanafunzi katika
shule hiyo iliyopo Hajipur, katika jimbo hilo lililopo mashariki ya jimbo hilo la Bihar.
Wazazi na marafiki wa wanafunzi walipigwa picha wakipanda
kuta za shule ili kupeleka majibu hayo kwa wanafunzi.
Mtu akimjibia maswali ya mtihani mwanafuzi kabla hajampekelea darasani huko India. |
Wengi waliokamatwa walikuwa wazazi. Karibu wanafunzi 750
wamefukuzwa shule kutokana na tukio hilo la kushangaza.
Inakadiriwa kuwa wanafunzi Milioni 1.4 walikuwa wakifanya
mitihani ya kumaliza shule huko Bihar pekee, huku ikionekana mitihani hiyo
ikiwa ni muhimu sana katika maisha yao.
Mamlaka ya jimbo hilo imesema kuwa, imesononeshwa sana na
udanganyifu huo wa mitihani.
Wanafunzi walionekana wakinakili majibu kutoka vikaratasi
walivyopewa, na polisi walitoa taarifa kuwa inaelekea hata vituo hivyo vyaa
mitihani vilipewa hongo ili kuruhusu hali hiyo.
Imeelezwa kuwa ni jambo la kawaida kufanywa kwa udangayifu
katika mitihani huko Saharsa Cheating is katika mitihani huko Bihar na
ilionekana wazi katika picha zilizopigwa.
Kiongozi mmoja huko Saharsa aliwaonya wazazi wasifanye
vitendo hivyo vya kuwasaidia watoto wao kudanganya katika mitihani.
Mbali na kukamatwa, vituo vine vya mitihani vimefutwa
kabisa.
Baadhi ya watu nchini India wakiwa katika harakati za kuwapelekea wanafunzi majibu ya mtihani. |
Waziri Kiongozi wa Bihar Nitish Kumar alilaani vitendo hivyo
vya udangayifu lakini alisema kuwa picha hizo sio hali halisi ya jimbo lake.
Aliwaonya wazazi kuwa vitendo vya kuwasaidia wanafunzi
kufanya udanganyifu katika mitihani kuna waharibu na wala hakuwajengi katika
maisha yao ya baadae.
Waziri wa Elimu ya India PK Shahi alisema itakuwa vigumu kuendesha
mitihani kwa haki bila ya kupata msaada kutoka kwa wazazi, alitoa idadi kamili
ya watu waliojihusisha na sula hilo.
Baadhi ya watu wakipanda ukuta kwenda kuwapelekea wanafunzi majibu ya mitihani katika jimbo moja la India. |
"Watu watatu hadi wanne walikuwa wakimsaidia mwanafunzi
mmoja ikiwa na maana kuwa, kulikuwa na jumla ya watu Milioni sita hadi saba
waliwasaidia wanafunzi kupata majibu ya mitihani, “ alisema.
"Kweli ni mujibu wa serikali peke yake kudhibiti
idadikubwa ya watu namna ile na kuendesha kwa asilimi 100 mtihani huru na wa
haki?"
No comments:
Post a Comment