Friday, 10 February 2017

Simba yapania kuifunga Tanzania Prisons leo na kuiondoa Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi KuuNa Mwandishi Wetu
SIMBA leo ina nafasi ya kuiengua Yanga kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, endapo itaifunga Tanzania Prisons katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wekundu hao wa Msimbazi wanahitaji ushindi kwa nguvu kwani lengo lao sio tu kuwaondoa watani zao kileleni, bali pia wanataka kulipa kisasi cha kufungwa na Prisons katika mzunguko wa kwanza katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.

Simba wako katika nafasi ya pili nyuma ya Yanga wakiwa na pointi 48 na kama wakishinda leo watafikisha 51 na kurejea katika kilele cha msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.

Yanga wenyewe leo hawatashuka dimbani kwani wako `angani wakienda Comoro kucheza na mabingwa wa huko Ngaya De Mbe katika mchezo utakaofanyika kesho Jumapili.

Kutoshuka uwanjani kwa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kunaipa mwanya Simba kushika usukani endapo wakishinda watafikisha pointi 49 na kuifikia Yanga.

Yanga watakuwa na mchezo mmoja pungufu, huku Simba baada ya mchezo wa leo itakuwa imefikisha mechi 22 na kubakisha nane kabla ya kufungwa kwa mbio hizo za ubingwa.

Ushindi wa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo umeongezeka mara dufu hasa baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kuwa mshindi wa kwanza ndiye atawakilisha taifa katika Ligi ya Mabingwa huku mshindi wa pili akitoka kapa.
 
Hatahivyo, Simba wasitarajie mteremko kwani Prisons wako vizuri na wanaingia uwanjani huku wakiwa wameshinda mechi mbili mfulululizo zilizotangulia,,kitu ambacho kinawafanya wawe na ari kubwa.

Prisons ilipata ushindi dhidi ya maasimu wao Mbeya City kwa mabao 2-0 kabla ya kuifunga 2-1 Ruvu Shooting na kuzidi kuwa na ari ya ushindi bila kujali timu itakayocheza nayo.

Mshindi wa Kombe la Mashindano ya Kombe la FA ndiye atakayeliwakilisha taifa katika mashindano ya Shirikisho la Afrika, hivyo kubakisha nafasi moja tu ya mshindi wa Ligi Kuu kushiriki Ligi ya Mabingwa wa Afrika, wakati huko nyuma mshindi wa pili wa Ligi Kuu alikuwa akishiriki Kombe la Shirikisho.

Mechi zingine za leo ni kati ya Azam FC itakayocheza dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini Mlandizi, huku Stand United ikiikaribisha Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga.

Toto Africans ya Mwanza ikaikaribisha JKT Ruvu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba wakati kesho African Lyon itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar na Mwadui ya Shinyanga watawakaribisha Mbeya City.

Msimamo:


MP
W
D
L
G
P
1
Young Africans
21
15
4
2
+37
49
2
Simba
21
15
3
3
+26
48
3
Azam
21
10
7
4
+10
37
4
Kagera Sugar
21
11
4
6
+4
37
5
Mtibwa Sugar
21
8
7
6
-2
31
6
Tanzania Prisons
22
7
8
7
-1
29
7
Ruvu Shooting
21
6
9
6
-3
27
8
Mbao
21
7
5
9
+0
26
9
Stand United
21
6
8
7
-2
26
10
Mbeya City
21
6
8
7
-2
26
11
Mwadui
21
7
4
10
-9
25
12
African Lyon
21
4
10
7
-6
22
13
Ndanda
21
5
5
11
-14
20
14
Toto Africans
21
4
6
11
-10
18
15
Maji Maji
21
5
3
13
-17
18
16
Ruvu Stars
22
2
11
9
-11
17

No comments:

Post a Comment