Monday, 6 February 2017

Manchester City haina mpango wa kumpiga bei mkali wake Sergio


Mshambuliaji Mbrazil wa Man City, Gabriel Jesus (katikati) akishangilia pamoja na beki Muargentina, Pablo Zabaleta (kushoto) na kiungo Mjerumani Leroy Sane (kulia) baada ya kufunga bao la ushindi la dakika za mwisho walipocheza dhidi ya Swansea City kwenye Uwanja wa Etihad Stadium jana. Man City ilishinda mabao 2-1.

 MANCHESTER, England
MANCHESTER City haina mpango wa kumuuza Sergio Aguero katika kipindi hiki cha Majira ya Joto, licha ya mshambuliaji huyo kutopangwa katika mechi mbili zilizopita.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alisaini kuongeza mkataba mapema mwaka huu, ikiwa na maana kuwa amebakiza miaka mitatu kabla ya kumaliza mkataba huo.

Baada ya kuingia akitokea benchi wakati Man City ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Swansea, Aguero alisema: "Bila shaka nataka kuendelea kubaki hapa.

"Katika miezi hii mitatu natakiwa kuisaidia klabu na wao ndio watakaoamua hatma yangu kama nitaendelea kuhitajika hapa au la.”
Kipa wa Manchester City, Willy Caballero akishangilia.
Licha ya Aguero kutarajia uamuzi kufanywa wakati wa kipindi cha majira ya joto, mmoja wa wazito katika klabu ya Man City alidokeza juzi kuwa hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina aliingia akitokea benchi wakati Man Cuty ikiibuka na ushindi mzuri dhidi ya Swansea shukrani kwa bao la ushindi la dakika za mwisho la Gabriel Jesus, la mchezo wa pili wa Mbrazil huyo, aliyechukua nafasi ya Aguero katika kikosi cha kwanza.

Aguero ndiye mfungaji anayeongoza kwa kufungamabao mengi Man City, ambapo msimu huu amefunga mabao 18, ikiwa 11 zaidi ya Raheem Sterling, ambaye anafuatia katika orodha hiyo.

Ni mchezaji wa tatu kufunga mabao mengi katika kipindi chote Man City akiwa na mabao 154 na alikuwa mshindi wa kiatu cha dhahabu katika Ligi Kuu katika msimu wa mwaka 2014-15.

Pia ndiye mfungaji anayeongoza kwa kupachika mabao katika msimu wa mwaka 2011-12 katika kampeni zake za kutwaa ubingwa.

No comments:

Post a Comment