Thursday, 9 February 2017

MICHAEL Ballack amtaka Ozil kuondoka Arsenal kama anataka matajiMUNICH, Ujerumani
MICHAEL Ballack ameshauri kuwa Mesut Ozil (pichani) anatakiwa kuondoka Arsenal na kujiunga na Bayern Munich, endapo anataka kushinda mataji.

Ozil amebakisha miezi 18 katika mkataba wake na the Gunners,ambaye anaonekana kuelekea kukosa tena taji la Ligi Kuu mwaka huu baada ya timu hiyo kuwa pointi 12 nyuma ya Chelsea.

Ballack alishinda taji la Ligi Kuu katika msimu wa mwaka 2009/10 akiwana the Blues, na aliliambia gazeti la Ujerumani la Bild kuwa Ozil anatakiwa kujiunga na Bayern ikiwa anataka kushinda mataji.

"Mesut ni mchezaji wa ajabu. Anajua kuwa ni mchezaji wa aina yake pale Arsenal, “alisema. “Klabu nying zitapendezwa kuwa naye.

"Anaishi London, moja ya miji mizuri zaidi…”

Arsene Wenger alisema Desemba kuwa Arsenal kamwe haina mpango wa kumuuza ama Ozil au Alexis Sanchez, hata kama watashindwa kuelewana katika mkataba mipya.

Lakini Ballack anasema Bayern itahitaji kujiandaa kutumia fedha zaidi ili kuwanunua wachezaji wakubwa

No comments:

Post a Comment