Wednesday, 8 February 2017

Madonna aongeza watoto mapacha Malawi ili kuwaasiliBLANTYRE, Malawi 

NYOTA wa muziki wa pop wa Marekani Madonna ameasili watoto wakike mapacha nchini Malawi juzi, kilisema chanzo kutoka mahakamani.


Mwanamuziki huyo sasa ana jumla ya watoto wanne aliowaasili kutoka nchini hiyo iliyopo Kusini mwa Afrika.
Wiki mbili zilizopita, mwanamuziki huyo nyota alikana kuhusishwa na kutuma maombi ya kutaka kuwaasili watoto nchini Malawi.

"Naweza kuthibitisha kuwa Madonna amehakikishiwa kibali cha kuwaasili watoto wawili mapacha, “alisema msemaji ea jaji Mlenga Mvula, ambapo alielezea kuwa ni mapacha wa miaka minne wanaitwa, Esther na Stella.

Wakati akielekea kutoa uamuzi wa kesi hiyo Jaji Fiona Mwale, muimbaji huyo alitua katika Mahakama Kuu iliyopo katika mji mkuu wa Lilongwe akiwa na walinzi kibao binafsi na polisi, vilisema vyombo vya habari vya hapa.

Madonna, ambaye alianzisha kituo cha kuchangia yatima kinachoitwa Raising Malawi mwaka 2006, awali aliwaasili watoto wawili nchini humo, David Banda mwaka 2006 na Mercy James mwaka 2009.

Hatahivyo, hakukuwa na taarifa zaidi kuhusu hatua hiyo ya mahakama.

Mwale alisema kuwa mapacha hao wanatoka katika Kituo cha Yatina cha Hope kilichopo Mchinji, mji wa magharibi uliopo jirani na mpaka wa Zambia amba uko kilometa 110 kutoka Lilongwe.

David Banda naye aliasiwa kutoka katika kituo hicho.

Wiki mbili zilizopita, Madonna,mwenye umri wa miaka 58, alikanusha taarifa kuwa ataenda katika mahakama hiyo hiyo kufungua maombi ya kutaka kuasili mtoto, akielezea gazeti la Watu kuwa "tetesi za kutaka kuasili mtoto sio za kweli.”

Mwaka 2013, nyota huyo wa muziki aliondolewa heshima ya Watu Mashuhuri na Serikali ya Rais wazamani wa Malawi, Joyce Banda, ambayo ilikuwa ikimtuhumu mwanamuziki huyo kuwa na tabia mbaya.

No comments:

Post a Comment