Sunday, 12 February 2017

Hatimaye Chama cha Tenisi chapata viongozi wapya, Mwasanga Katibu Mkuu wake mpyaNa Gilbert Peter
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Kamati ya Olimpiki Tanzania, Irene Mwasanga ameshinda ukatibu mkuu wa Chama cha Mpira wa Tenisi Tanzania (TTA).

Katika uchaguzi huo mkuu uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Mwasanga ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake ya Kamati ya Olimpiki za Afrika, aipata kura 15 za ndio.

Rais wa mpya wa TTA ni Dennis Sirito Makoi aliyepata kura za ndio 16 wakati makamu wake ni John Bura aliyepata kura 16.
 
Walioshinda katika nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TTA, ni pamoja na Mosses Mabula aliyepata kura 13, Rehema Mbegu aliyepata kura 16, Rizik Salum Seleman kura 15.

Wengine walioshinda nafasi hizo za ujube wa Kamati ya Utendaji ni pamoja na Sanjay Choksh alipata kura 13.
 
Uchaguzi huo uliosimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) umefanyika baada ya TTA kutokuwa na viongozi kwa muda baada ya baadhi ya kuachia ngazi kwa sababu tofauti.

Aidha, viongozi hao wapya wana kibarua kizito kuhakikisha wanalipa madeni kibao yaliyoachwa na uongozi uliopita pamoja na kuuendeleza mchezo huo.

No comments:

Post a Comment