Thursday, 23 April 2015

Mabilionea wabana matumizi kwa kukaa `kajamba nani' katika ndege



Wakinaswa na kamera: Kanye West na Kim Kardashian walipigwa picha wakiwa wameuchapa usingizi katika economy class wakati wakisafiri kwenda Armenia mapema mwezi huu.

NEW YORK, Marekani
INAKADILIWA kuwa wana utajiri wa pamoja wenye thamani ya dola za marekani Milioni 155 (ambao ni sawa na Tsh. 279,000,000,000).

Lakini pamoja na utajiri huo, matajiri na watu maarufu kumbe nao wakati mwingine hubana matumizi ili kusevu kiasi fulani cha fedha wakati huo, ambapo Kim Kardashian na Kanye West walifanya hivyo kwa kupanda daraja la `economy’ ni sawa na daraja la tatu katika treni au kama inavyojulikana sana kama 'kajamba nani?`wakati wakisafiri kwa ndege kwenda Armenia mapema mwezi huu.

Mbali na daraja hilo la chini (economy class), katika ndege huwa na madaraja mengine kama Bussiness Class, ambalo ni la wastani na lipo kati ya economy na lile la first class (ambalo ni la juu kabisa), lakini ndege nyingi  siku hizi business class ndilo daraja la juu zaidi, baada ya kuondoa sehemu ya daraja la kwanza.

Business Class linatofautishwa na madaraja mengine kutokana na ubora wa viti vyake, chakula, vinywaji na huduma zingine.



Huwezi kubashiri kama  Kim alitumia muda wote katika ndege akiwa katika economy class wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa  Zvartnots huko Yerevan, Armenia 
Nyota hao walionekana wakichapa usingizi katika sehemu hiyo ya `economy ambayo unakaa au kulala kwa shinda katika viti vya eneo hilo, tofauti na ilivyozoeleka ambapo watu maarufu kama hao wamekuwa wakikaa katika daraja la kwanza, ambako wanapata huduma za VIP.

Picha zilizotumwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter, zinawaonesha wawili hao wakijaribu kupiga usingizi pamoja na abiria wengine katika daraja hilo ambalo linaitwa `cattle class.

'Kim & Kanye walisafiri katika daraja la Economy kwenda Armenia (sic)', Maili na maili, ambapo maelezo ya picha yalieleza hivyo kuhusu wapenzi hao wapya.

Kim alionekana akiwa amelala katia kiti chake akiwa amejifunika koti ambalo lilimfukika kama blanketi.

No comments:

Post a Comment