Sunday, 21 June 2015

Kipigo Taifa Stars chasababisha kocha kutupiwa virago



Na Mwandishi Wetu Zanzibar
KAMATI ya Utendaji ya Shirikishi la Soka Tanzania (TFF) imemtimua kocha wa Taifa Stars, Mholanzi, Mart Nooij na habari zinasema, kocha msaidizi wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa atashika timu kwa muda, akisaidiwa na Suleiman Matola wa Simba SC. 

Kamati ya Utendaji ya TFF ililazimika kufanya kikao cha dharula baada ya Stars kufungwa mabao 3-0 na Uganda usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mchezo wa kwanza raundi ya kwanza kufuzu CHAN 2016. 

Katika kikao cha leo (jana), pamoja na mambo mengine ilipitia mwenendo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu,imesema taarifa ya TFF.

Kamati ya utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo: 1.Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia  tarehe 21/June/2015. 

2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia tarehe 21/06/2015.

3.Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa,imemalizia taarifa hiyo fupi iluyitolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya TFF, Baraka Kizuguto.

Lakini mara baada ya mchezo huo, Nooij alisema hawezi kuondoka kwa matokeo ya uwanjani, kwa sababu ana mkataba hadi mwaka 2016.

TFF italazimika kumlipa Nooij dola za Kimarekani zisizopungua 125, 000 (Sh. Milioni 250,000) kwa kumvunjia mkataba, ambao ni mishahara yake ya miezi 10, kwa sababu kwa mwezi alikuwa analipwa dola 12,500 (Sh. Milioni 25).

Mabao mawili ya mshambuliaji Erisa Sekisambu na lingine la Farouk Miya yanahitimisha historia ya kocha huyo Mholanzi Tanzania.

Habari za ndani zinasema Mkwasa na kocha Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola watapewa timu kwa muda- mtihani wao wa kwanza ukiwa ni kujaribu kushinda mabao 4-0 ugenini wiki mbili zijazo ili kusonga mbele CHAN.

Matokeo ya jana yamewakosesha wachezaji wa Taifa Stars donge nono la Sh. Milioni 1 kila mmoja ahadi iliyotolewa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Mchezo wa leo unakuwa wa tano mfululizo, Taifa Stars inafungwa chini ya Nooij aliyerithi mikoba ya Mdenmark Kim Poulsen Aprili mwaka jana na kwa ujumla timu hiyo imecheza mechi tisa bila ya ushindi chini ya Mholanzi huyo. 

Kwa ujumla, Nooij ameiongoza Stars katka mechi 18 tangu arithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen Aprili mwaka jana, kati ya hizo ameshinda tatu tu, sare sita na kufungwa tisa- akifunga mabao 17 na kufungwa 28.

Saturday, 20 June 2015

Taifa Stars yafungwa na Uganda, kocha akaribia kutupiwa virago



 *Aondolewa chini ya ulinzi mkali wa polisi akihofia kupigwa

Na Mwandishi Wetu Zanzibar
SAFARI ya Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeiva baada ya leo usiku timu yake kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa majirani zao wa Uganda katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Chan 2016.

Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (Chan), zitafanyika mwakani nchini Rwanda na Tanzania imecheza na Uganda `The Cranes kujaribu kusaka nafasi hiyo katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilimpa kocha Mart Nooij mtihani wa mwisho na endapo atashindwa kuipeleka Taifa Stars, basi atafute njia ya kuondoka baada ya wapenzi wa soka nchini kuchoshwa na ipigo ya timu hiyo.

Wiki iliyopita, Taifa Stars ilipokea kichapo cha idadi kama hiyo cha mabao kutoka kwa Misri katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Gabon.

Kocha wa rtimu ya taifa ya Tanzania (kushoto) akisindikizwa na polisi mara baada ya filimbi ya mwisho timu yake ilipocheza na Uganda Cranes kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar Polisi hao walikuwa wakimlinda asiadhibiwe na wapenzi wa soka wenye hasira.
Hakuna ubishi kuwa baada ya kichapo hicho cha leo kocha huyo Mholanzi atajiongeza kabla TFF haijamuonesha njia ya kutokea baada ya mchezo wa pili utakaofanyika Kampala Uganda wiki mbili zijazo.

Mwaka jana Tanzania ilifungwa 1-0 na Uganda katika mchezo kama huo wa Chan uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa kabla ya kutolewa na kuiacha The Cranes ikisonga mbele.

Mabao ya The Cranes katika mchezo huo ulioanza saa 2;30 usiku ili kuwawezesha wapenzi wa soka kufuturu ndio waende uwanjani yalifungwa na Sekisambo Erisa mabao mawili na Miya Farouk.

Kabla ya kuanza mchezo huo, Taifa Stars ilipata pigo baada ya mchezaji wake Oscar Joshua kuugua gafla na kuukosa mchezo huo.

Kwa mara ya mwisho Stars ilifuzu kwa fainali hizo za Chan mwaka 2009 zilipofanyika kwa mara ya kwanza nchini Iory Coast na ilitolewa katika hatua ya makundi ikiwa chini ya Mbrazil Marcio Maximo.

Wakati huohuo kocha wa timu hiyo ilibidi asindikizwe na polisi mara baada ya filimbi ya mwisho ili kumzuia asipate kichapo kutoka kwa mashabiki wenye hasira waliotaka kumpifa.


Friday, 19 June 2015

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege atembelea banda lao

Mkurugenzi wa TAA, Suleiman Suleiman (kulia) akihojiwa katika banda la mamlaka hiyo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo.


Banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Baadhi ya vifaa ambavyo haviruhusiwi kuingia navyo katika ndege vikioneshwa katika banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Suleiman Suleiman akizungumza na waandishi wa habari katika banda la TAA la maonesho ya Wiki ya Utumisi wa Umma.
Ofisa Usalama Mwandamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Bakari Mwalwisi (kushoto), akitoa maelezo ya usalama kwa wananchi waliotembelea banda hilo la maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Wednesday, 17 June 2015

Maonesho Wiki ya Utumishi wa Umma yaendelea Mnazi Mmoja


Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, Mabele Masasi (kulia), akitoa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea banda lao leo kwenye viwanja wa Mnazi Mmoja.

Msanii mahiri nchini Mrisho Mpoto (kulia), ambaye ni balozi wa PSPF akiwa katika banda la taasisi hiyo leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.

Baadhi ya wananchi wakiangalia samaki katika banda la Magereza kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.

Thadeo azindua Airtel Tanzania Rising Stars


Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Leonard Thadeo akipiga mpira kuashiria kuanza kwa mashindano ya Airtel Rising Stars.

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania jana ilizindua rasmi msimu wa tano wa mashindano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ambayo yataanza kutimua vumbi Agosti 8 katika ngazi ya awali na kuhitimishwa kwa fainali za Taifa Dar es Salaam kuanzia Septemba 11 – 21 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi huo jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kampuni ya Airtel Tanzania  ina nia thabiti ya kusaidia maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini na kujivunia mafanikio yaliyotokana na michuano hiyo kwa miaka minne iliyopita.

 “Tunaona fahari kwamba michuano ya Airtel Rising Stars imeweza kuibua vipaji vya wachezaji ambao baadhi yao wamechaguliwa kujiunga na timu za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 20”, alisema Singano.

Kumbukumbu za TFF zinaonyesha kwamba timu ya taifa ya wanawake imeundwa na wachezaji wengi kutoka Airtel Rising Stars ambayo madhumuni yake makubwa ni kuibua na kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17. 

Singano pia ametangaza kampuni ya Airtel kuingia mkataba na nahodha wa Ivory Coast na kiungo wa Manchester City Yaya Toure katika kampeni mpya iitwayo  “It’s Now” yenye lengo la kulea na kukuza vipaji barani Afrika kupitia Nyanja mbalimbali kama vile michezo, ikijumuisha mashindano ya Airtel Rising Stars kwa vijana chini ya umri wa miaka 17.

Alisema sehemu nyingine ambazo kampeni hii itazigusa ni mtindo wa maisha na muziki, ambapo wateja watapata ufumbuzi wa masuala mbalimbali ya kiteknolojia ili kuona fursa zinazowazunguka.

Huu ni mwaka wa tano mfululizo kwa michuano ya Airtel Rising Stars kufanyika hapa nchini Tanzania ambayo huanzia ngazi ya chini hadi Taifa. Singano alilipongeza Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) pamoja na serikali kupitia Wizara ya Michezo kwa kuiunga mkono kwa dhati michuano ya Airtel Rising Stars tangu ilipoanzishwa nchini mwaka 2011.

Mkurugenzi wa Idara ya michezo katika wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema serikali inatambua mchango wa Airtel katika kuibua vipaji vya wanasoka chipukizi. 

“Inatuwia vigumu kuwekeza kikamilifu katika michezo kwa sababu ya kuelemewa na majukumu mengine muhimu ya kijamii ndio maana tunahamasisha sekata binafsi kujitokeza kusaidia na Airtel wanafanya kazi nzuri,” alisema Thadeo.     

Mwaka huu michuano ya ARS itajumuisha mikoa ya Ilala, Kinondoni,Temeke Mbeya, Mwanza na Morogoro kwa upande wa wavulana na huku upande wa wasichana ukiwakilishwa na mikoa ya Ilala,Kinondoni, Temeke, Mbeya na Arusha.

Kwa upande wake, Rais wa TFF Jamal Malinzi aliipongeza Airtel Tanzania kwa kuwekeza kwenye soka la vijana. “Nawapongeza sana kampuni ya Airtel Tanzania kwa mpango wake huu wa kuwekeza kwenye soka la vijana ambao kwa kweli ndio msingi wa maendeleo wa mpira wa miguu hapa Tanzania na duniani kote”, alisema.

Tuesday, 16 June 2015

Watu wenye hasira walipopomoa mawe basi la TFF

Basi la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), likiwa limevunjika kioo baada ya watu wenye hasira kukivunja jana wakichukizwa na timu hiyo kufungwa 3-0 na Misri katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2017. Picha hiyo imepigwa leo wakati likiwa limeegeshwa katika hoteli moja jijini Dar es Salaam.
Kioo ambacho kimevunjwa na watu wenye hasira cha basi la TFF.

Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalivyoanza Mnazi Mmoja leo

Banda la Muhimbili wakikamilisha maandalizi ya mwisho wakati wa maonesho ya Utumishi wa Umma leo.

Mabanda ya taasisi mbalimbali wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo.
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Frida Nkondokaya (kushoto) akitoa maelezo ya huduma wanazotoa katika taasisi yao wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa umma leo.
Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bahati Mollel (kulia) na mfanyakazi mwenzake wa mamlaka hiyo, Frida Nkondokaya wakitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda la TAA leo, siku ya kwanza ya maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.




Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakitoa maelezo kwa watu waliotembelea banda lao jana siku ya kwanza ya wiki ya maonyesho ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo.

Siku ya Mtoto wa Afrika ilivyofana Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam

Wanafunzi wa shule ya msingi ya Madenge wakiendesha Bunge maalum la watoto wakati wakiadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika leo kwenye viwanja vya Mwembe Yanga.
Baadhi ya washiriki wa Siku ya Mtoto wa Afrika mkoa wa Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwembe Yanga leo Jumanne, Juni 16.

Spika wa Bunge la Watoto, Zubeda Yussuf  (wa pili kulia), wa shule ya msingi Madenge iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam leo., akitoka baada ya kuendesha kikao wakati wa Siku ya Watoto Mwembe Yanga.
Wanafunzi wakicheza mchezo wa kuigiza kuhusu ndoa za utotoni wakati wa kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika leo katika viwanja vya Mwembe Yanga.
Wanafunzi wakicheza wakati wa Siku ya Mtoto wa Afrika jijini Dar es Salaam jana.

Kongamano la Saba la Ramadhani lafanyika jijini Dar es Salaam

Mshindi wa kwanza wa kusoma Qurani Tukufu Tanzania na mshndi watano duniani 2014, Mohamed Boki akisoma Qurani wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Saba la Ramadhani kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kongamano hilo ni mahsusi kwa ajili ya kuukaribisha mwezi Utukufu wa Ramadhani.


Brother Mussa Azir akisoma dua wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Saba la Ramadhani.
Sheikh Mohamed Mussa alikuwa mmoja wa wazungumza katika Kongamano la Saba la Ramadhani lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dr. Muhsin Masoud akizungumza wakati wa Kongamano la Saba la Ramadhani lililofanyika jijini Dar es Salaam. Amana Bank ndio benki ya kwanza nchini kufuata misingi ya Kiislamu hapa nchini.
Mzungumzaji Mkuu wa Kongamano la Saba la Ramadhani, Dr. AhmaTotonji akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Saba la Ramadhani lililofanyika jijini Dar es Salaam.