Monday 25 July 2016
Wednesday 20 July 2016
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi uwanja wa ndege Dodoma
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
MAMLAKA YA
VIWANJA VYA NDEGE
Simu: +255 22 2842402-3 S.L.P 18000,
Fax: +255 22 2844495 DAR
ES SALAAM
19/07/2016
E-mail:info@airports.go.tz
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Kassim M. Majaliwa kesho, tarehe 20/07/2016, anatarajiwa
kuweka jiwe la msingi la mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha ndege cha
Dodoma.
Ukarabati huo utajumuisha
urefushaji wa barabara ya kuruka na kutua ndege hadi kufikia urefu wa kilometa 2.5
kutoka Kilometa 2 za awali.
Kurefushwa kwa barabara
hiyo, sasa kutatoa fursa kwa ndege kubwa Bombardier Q400, Gulfstream 550, ATR
72 n.k zenye uwezo wa kubeba abiria 90.
Ukarabati huo unafanyika kwa
fedha za Serikali ya Tanzania na unasimamiwa na Wahandisi wa Mamlaka ya Viwanja
Vya Ndege Nchini kwa ushirikiano na Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS).
Ukarabati na upanuzi wa
Kiwanja cha Ndege cha Dodoma ni miongoni mwa Miradi mbali mbali inayotekelezwa na
Mamlaka ya viwanja Vya Ndege nchini kama vile Viwanja vya Tabora, Bukoba,
Kigoma na Mwanza ambayo imekwisha anza na miradi mipya ya viwanja vya ndege vya
Shinyanga na Sumbawanga itakayoanza hivi karibuni.
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA) ni wakala wa viwanja vya ndege iliyoanzishwa kwa Tangazo la
Serikali Namba 404 la mwaka 1999, chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya
mwaka 1997.
Dira:
Kuwa mtoaji wa Huduma za Viwanja vya Ndege kwa
kiwango cha Kimataifa
Dhima:
Kutoa Huduma Bora na Viwezeshi katika Viwanja vya
Ndege kwa kuzingatia ufanisi katika matumizi ya rasilimali zilizopo
Imani kuu za Mamlaka:
·
Kuwajali
Wateja
·
Kuwaendeleza
Wafanyakazi wa Mamlaka
·
Ulinzi
na Usalama Viwanjani
·
Kufanya
kazi kwa pamoja
·
Kuwa
na Uongozi wa Mabadiliko
·
Uadilifu
IMETOLEWA NA KITENGO CHA SHERIA
NA MAHUSIANO TAA
Monday 11 July 2016
Caf yaipiga faini yanga ya milioni 10 kwa wachezaji wake kumzonga mwamuzi walipocheza na timu ya Angola
Na Mwandishi Wetu
KLABU ya Yanga imesema kuwa inatafakari adhabu ya dola
5,000 (sawa n ash milioni 10) waliyopigwa na Shirikisho la Soka la Afrika (Caf)
baada ya wachezaji wake kuchelewesha muda.
Caf juzi ilitangaza kuiadhibu Yanga baada ya baadhi ya
wachezaji wake kumzonga mwamuzi na kusababisha kuchelewesha mchezo wake timu
hiyo ilipocheza na GD Sagrada Esperanca uliofanyika Angola Mei 18, 2016.
Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit anakiri
wachezaji wao kumzonga mwamuzi lakini kwa sasa wanatafakari kabla ya kutoa
tamko kamili.
Mchezo huo ulikuwa ni wa hatua ya kutafuta nafasi ya
kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika.
Uamuzi wa mchezo huo Na. 100 ulifanywa na Kamati ya
Nidhamu ya CAF inayoundwa Mwenyekiti Raymond Hack –
Raia wa Afrika Kusini na wajumbe Mustapha Samugabo (Burundi) na Gbenga
Elegbeleye (Nigeria). Pia alikuwako Amina Kassem kutoka Sekretarieti ya CAF
ambaye ni Mtawala
katika Kitengo cha Nidhamu.
Katika mkutano huo uliofanyika Cairo, Misri –
Makao Mkuu ya CAF, Julai 3, 2016, kamati ilipitia taarifa zote za mchezo na
kufikia uamuzi wa kuipiga faini Yanga.
Taarifa za mchezo zinasema, wachezaji wa timu hiyo walionesha
utovu wa nidhamu kwa kumzonga mwamuzi na kumsukuma mara baada ya kutoa adhabu
ya penalti kwa wapinzani.
Kwa tukio hilo, mchezo huo ulisimama kwa dakika sita.
Polisi waliingia uwanjani kudhibiti hali hiyo.
Kwa kosa hilo, Wachezaji wa Yanga walivunja Ibara ya
82 inayozungumza utaratibu wa mawasiliano. Kwamba chama chochote cha mpira wa
miguu, klabu, ofisa au mtu yoyote wakiwamo wachezaji, lazima waheshimu
utaratibu za kuvumilia, uadiliufu na uanamichezo.
Kwa mujibu wa Kamati hiyo ya Nidhamu ya CAF, Yanga ilistahili
kutozwa faini ya dola 10.000 za Marekani kwa makosa ambayo si uungwana kwenye
soka yaliyoonyeshwa na wachezaji wake.
Lakini kwa kuwa Yanga haikuonyesha utovu wa nidhamu
katika mchezo mingine ya kimataifa iliyofuata dhidi ya MOB ya Algeria na TP
Mazembe ya DRC, imepunguziwa adhabu na sasa wametakiwa kulipa dola 5,000 za
Marekani kama faini.
Faini hiyo haina budi kulipwa mara moja. Na imetakiwa
kuendelea kuwa na nidhamu, vinginevyo adhabu hiyo itawarudia.
Wachezaji yanga walivyopamba utoaji zawadi kwa washindi wa American Super Market
Na Mwandishi Wetu
WACHEZAJI wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga
jana walisimamisha kwa muda shughuli American Super Market walipotinga katika
hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa draw iliyoendeshwa na duka hilo.
Baadhi ya wachezaji hao walioongozwa na nahodha
wao, Haroub Cannavaro ni pamoja na Donald Ngoma, Geofrey Mwasuiya, Malim
Busungu, Donald Ngoma na Juma Abdul.
Wachezaji wa Yanga walipowasili American Super Market. |
Wachezaji hao waliongozana na meneja wa timu hiyo,
Hafidh Busungu.
Katika hafla hiyo, wachezaji wa Yanga Cannavaro na
wengine walitoa zawadi kwa washindi wa pili na tatu,
Meneja wa Yanga, Hafidh Ally (kulia) akiwa na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo. |
Meneja wa timu hiyo Hafidh katika `waliteka’
kwa muda ASKARI wa Kikosi cha Jeshi cha 831 Mgulani JKT, luteni Reajero Mirambo
ametwaa pikipiki baada ya kuibuka wa kwanza katika shindano la American Super
Market (ASM)juzi.
`Mjeda’
huyo alikabidhiwa pikipiki hiyo yenye thamani ya sh milioni 1.4 aina ya Fighter
katika hafla iliyofanyika katika duka hilo lililopo Quality Centre, Dar es
Salaam na kuhudhuriwa pia na baadhi ya wachezaji wa Yanga.
Mshindi watatu, Neema Mosha akipokea jezi iliyosainiwa na wachezaji wa Yanga. Katikati ni Peter Minja meneja mahusiano wa Quality Group. |
Baadhi ya wachezaji hao wa Yanga wakiongozwa na
nahodha wao, Nadir Haroub Cannavaro, walikabidhi zawadi kwa washindi hao,ambao
walioshinda kutokana na bahati nasibu iliwashindanisha wanunuzi wa bidhaa
zinazouzwa dukani hapo.
Mshindi wa pili wa shindano hilo, ambalo
liliwashindanisha wateja wa ASM walionunua bidhaa za kuanzia sh. 100,000 ni
Alex Munishi aliyepata mpira, ambao aliutoa hapo hapo kwa mtoto wake ambaye ni
kipa wa Yanga, Deo Munishi au Dida.
Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub Cannavaro (kulia) akimkabidhi mpira mshindi wa pili, Alex Munishi. Katikati ni meneja mahusiano wa Quality Group, Peter Minja. |
Mshidi watatu alikuwa mwanadada, Neema Mosha ambaye
ni shabiki wa Simba na alipata jezi ya Yanga iliyosainiwa na wachezaji wote wa
timu hiyo.
Katika hafla hiyo, mshindi wa kwanza ambaye
alikabidhiwa pikipiki aina ya Fighter yenye thamani y ash. milioni 1.4, ni
askari jeshi mwenye cheo cha luteni kutoka 831 KJ, Reajero Mirambo.
Mshindi wa kwanza, luteni Reajero Mirambo akizungumza na waandishi wa habari. |
Mirambo akizungumza baada ya kukabidhiwa pikipiki
hiyo alisema kuwa, itamsaidia kuondoa tatizo la usafiri akienda na kurudi
kazini kwake au wakati wa shuguli zingine kutokana na msongamano wa magari
jijini Dar es Salaam.
Washindi hao walipatikana baada ya kununua bidhaa
za kuanzia sh 100,000 na kuendelea, ambapo moja kwa moja waliingizwa katika
draw na kupatikana washindi hao watatu.
Sunday 10 July 2016
Saturday 9 July 2016
Ureno yaivaa Ufaransa katika fainali ya Mataifa ya Ulaya ya euro 2016 kesho Jumapili
PARIS, Ufaransa
BEKI wa kushoto mwenye kipaji, Raphael Guerreiro ni mmoja kati ya
wachezaji watatu wa Ureno ambao watakaikabili nchi yao waliyozaliwa, wakati
watakapokutana na Ufaransa kwenye fainali ya mataifa ya Ulaya, Euro 2016, kesho Jumapili saa nne usiku kwa saa za hapa Bongo.
Guerreiro na golikipa, Anthony Lopes walizaliwa na kukulia nchini
Ufaransa, ambako ni nyumbani kwa Wareno wengi wahamiaji.
Kiungo Adrien Silva aliishi nchini Ufaransa hadi akiwa na umri wa
miaka 12, wakati alipohamia nchini Ureno na familia yake.
“Nilichagua
Ureno. Yalikuwa maamuzi yangu muhimu. Si familia yangu wala marafiki zangu
ambao waliweza kuubadilisha uamuzi wangu,” amesema Guerreiro
mwenye umri wa miaka 22, ambaye mwezi uliopita alikubali uhamisho wa kwenda kwa
miamba ya Ujerumani, Borussia Dortmund akitokea Klabu ya Lorient inayoshiriki
Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1.
Guerreiro alizaliwa kitongoji cha Le Blanc Mesnil jijini Paris, umbali
mfupi kutoka kwenye Uwanja wa Stade de France ambako fainali hiyo inachezwa leo.
Ufaransa inaingia kwenye mchezo huo ikiwa ni nchi ya kwanza kufika
mara mbili fainali ya Euro ikiwa nchi mwenyeji wa mashindano, mara ya kwanza
ilikuwa mwaka 1984.
Michel Platini bado anashikilia rekodi ya magoli mengi zaidi
kwenye msimu mmoja wa michuano ya Euro (magoli 9, Euro 1984) magoli matatu
zaidi ya Antoine Griezmann aliyefunga magoli 6 hadi sasa Euro 2016.
Kwa upande wao Ureno hadi wanamaliza hatua ya makundi walikuwa
hawajashinda mchezo hata mchezo mmoja. Ni mfumo tu wa mashindano ya mwaka huu
ndiyo uliwapa nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora, kupitia mlango wa nyuma.
Ureno mechi yao katika hatua ya 16 bora ilishuhudia dakika 90
zikiisha kwa sare. Bao la ushindi likapatikana dakika ya 117, dakika tatu kabla
ya dakika za nyongeza kumalizika.
Ureno kwenye hatua ya Robo fainali waliitoa Poland kwa mikwaju ya
penalti baada ya sare ya bao 1-1 dakika 120.
Cristiano Ronaldo ameifikia rekodi ya gwiji wa Ufaransa, Michel
Platini ya kufunga magoli 9 ya Euro. Ronaldo alifunga goli lake la kwanza
kwenye michuano ya Euro mwaka 2004.
Anahitaji goli moja ili kuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye
michuano ya Euro.
Mara ya mwisho timu kutinga fainali kiujanja ujanja namna hii kama
Ureno, ilikuwa Italia kwenye kombe la Dunia 1982 na ikawa bingwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)