Thursday, 2 June 2016

Wafanyakazi Mamlaka wa viwanja vya ndege Tanzania (TAA) wafanya usafi Kigilagila kuelekea Siku ya Mazingira DunianiMkurugenzi wa Utawla na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Laurent Mwigune (kushoto) na mfanyakazi wa mamlaka hiyo, Veronica Rugaba wakati wakifanya usafi leo Kigilagila jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
WAFANYAKAZI wa Makao Makuu ya Mamlaka wa Viwanja vya Ndege (TAA), wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Laurent Mwigune  leo wamefanya usafi eneo la Kigilagila  jirani na Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa JK Nyerere.

Wafanyakazi hao walishirikiana na wakazi wa eneo hilo kufanya usafi katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani itakayofanyika Jumapili Juni 5.

Ofisa Usalama wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, Thomas Kimata aliwataka wananchi kutunza mazingira yanayowazunguka ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko yanayoweza kuwaambukiza kutokana na uchafu.

Hayo aliyasema wakati wafanyakazi wa mamlaka hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Laurent Mwigune wakifanya usafi katika eneo la Kigilagila jirani na Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa JK Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

Ofisa Usalama kutoka Makao Makuu ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Thomas Kimata akizungumza wakati wakifanya usafi Kigilagila leo.
Kimata aliwataka wananchi wa Kigilagila kuwa na mazoea ya kufanya usafi na kuacha kutupa taka jirani na ukuta wa uwanja huo kwani kufanya hivyo kunaziba mifereji na kuzuia maji kupita na kujaa katika maeneo ya uwanja huo.

Alisema kuwa wameamua kufanya usafi katika eneo hilo ikiwa ni sehemu yao ya kuelimisha jamii umuhimu wa usafi wakati tukielekea kuadhimisha Siku ya Mazingira duniani itakayofanyika Juni 5 Jumapili.

Baadhi ya wafanyakazi wa TAA wakifanya usafi leo Kigilagila jijini Dar es Salaam.
Alisema ni wajibu wao kutoa elimu kwa wananchi wanaozunguka uwanja huo ili wasiendelee kutupa taka katika maeneo hayo na mazingira yao, kwani itasaidia kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko.
Mtendaji wa Kigilagila aliwataka wananchi wa eneo kwa kushirikiana na polisi shirikishi kulinda eneo hilo ili watu wasitupe takataka.

Alisema kuwa kutupa uchafu katika eneo hilo kunaweza kusabbaisha kuanguka kwa ukuta wa uwanja huo wa ndege, hivyo aliwaacha kutofanya hivyo.

Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Vitula, Mary Jailos.
Mary Jailos, Mtendaji wa Mtaa wa Vituka zoezi hilo la usafi ni endelevu na litakuwa likifanya mara kwa mara ili kuhakikisha wananchi wa eneo hilo wanaishi katika mazingira yenye usafi.
Katika usafi huo, TAA ilitoa gari la takataka ambalo lilisomba taka zote katika eneo hilo, ambalo wananchi wa Kigilagila walifanya dambo dogo.

Mtendaji wa Kigilagila, Janeth Shepea.
Baadhi ya wananchi walisema kuwa TAA imefanya jambo zuri kufanya usafi na kuleta gari la taka kuzoa taka hizo na kuahidi kuwa watakuwa walinzi wa eneo hilo na kuhakikisha wenzao hawatupi uchafu.

Mmoja wa wananchi hao, Juma Bakari alisema kuwa, TAA imeonesha ujirani mwema na wao watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha mazingira yanayouzunguka uwanja huo wanayalinda.
 

No comments:

Post a Comment