Monday, 17 September 2018

IAMCO Washuhudia Panya Wakigundua Mabomu Ardhini

Lango la Kuingilia katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), ambako ziliko ofisi za Apopo, ambazo hutoa mafuno kwa panya kunusa harufu ya mabomu na kuibaini ugonjwa wa Kifua Kikuu.
Pendo Msegu, mmoja wa walimu wa panya jinsi ya kubaini mabomu yaliyofukiwa ardhini akiwa kaini leo SUA Morogoro.
Panya akisaka bomu lilikofukiwa .

 
Wanafunzi wa Institute of Arts and  Media Communication wakipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mawasiliano wa Apopo,  Lily Shallom  kuhusu wanavyowatunza na kuwapa mafunzo panya hadi kuweza kubaini mabomu yalipofukiwa ardhini. Kushoto ni Mkurugenzi wa chuo hicho, Ngayoma mjini Morogoro.

Mwanafunzi wa Iamco baada ya kuiva katika somo la upigaji picha akipata shot wakati walipotembelea Apopo mjini Morogoro leo.

 
 
Pendo Msegu, mmoja wa walimu wa panya akimrudisha panya katika banda lake baada ya kumaliza kumpima uzito. Panya hao kila asubuhi kabla ya kuanza mafunzo hupimwa uzito na wale wanaogundulika kuongezeka, hufanyishwa mazoezi na kupewa chakula maalum ili wapungue na kuwawezesha kufanya kazi vizuri, tofauti na wakiwa wanene.

KAMBI YA RIADHA YA DStv YAZINDULIWA MBULU



Makamu wa Pili wa Rais RT Ufundi, Dk Hamad Ndee (kulia), Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday (wa pili kushoto), mwanariadha waamani, Mzee John Stephen Akhwari (wa pili kulia) na  Mkuu wa Mawasiliano MultiChoice Tanzania, Johnson Mshana Mbulu mwishoni mwa wiki.

Ni katika maandalizi ya kuiletea Tanzania medali kwenye michezo ya kimataifa

Vijana 16 waanza kupikwa katika kambi hiyo maalum iliyopo Mbulu

•Wanariadha wakongwe wapongeza, Tanzania sasa kurejea kuwa kinara

MultiChoice Tanzania ikishirikiana na klabu yariadha ya Rift Valley ya Karatu imefungua kambi maalum ya raidha wilayan iMbulu ambapo wanariadha 16 watakuwa wakipati wa mafunzo kwa mwaka mzima.

Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na mwanariadha mwenye sifa ya kipekee duniani John Stephen Akhwari, katibu mkuu wa Shirikisho la RiadhaTanzania (RT), Wilhelm Gidabuday na Makamu wa Pili wa Rais wa RT (Ufundi), Dk. Hamad Ndee.

Kambi hiyo ina wanariadha wengi wenye umri mdogo, akiwemo Francis Damiano Damas, ambaye ni balozi maalum wa DStv na mshindi wa medali ya shaba katika mashindano ya vijana ya Jumuia ya Madola yaliyofanyika visiwa vya Bahamas mwaka jana.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Mkuu wa Mawasiliano MultiChoice Tanzania, Johnson Mshana, amesema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha kuwa riadha ina kuwa na mchango mkubwa katika kuliletea taifa sifa,  kutoa ajira kwa vijana wengi na kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi.
 
“Tunataka Tanzania ijulikane ulimwenguni kote kama chimbuko la mabingwa.Tumedhamiria kikamilifu kukuza mchezo huu na kufanya kama chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana wetu, lakini pia riadha ni mchezo, burudani na ni sekta nyeti kiuchumi kama ikiendelezwa.” 

“Tunataka kuusikia wimbo wetu wa  taifa katika mashindano makubwa ya riadha ya kimataifa, tunataka kuiona bendera yetu ikipepea juu katika kila mashindano makubwa ya riadha ya kimataifa ,tunataka mamia ya vijana wetu wenye uwezo mkubwa katika riadha washiriki kwenye mashindano makubwa, waweze kujipatia kipato na kuwachanzo cha maelfu ya ajira na hatimaye kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi ya nchiyetu,” amesema Mshana.
 
Kambi hii ilianza rasmi tarehe 1 Septemba 2018 na itasimamiwa na klabu ya Riadha ya Rift Valley kwa ufadhiliwa  Kampuni ya MultiChoice Tanzania, kwa mujibu wa makubaliano kati ya pande hizo mbili.

Kwa kuanzia kambi hiyo ina jumla ya  wanariadha 16 ambapo awamu ya kwanza ya mafunzo itakuwa kwa miezi mitatu (Septemba – Novemba 2018) na awamu ya pili (Januari- Machi 2019).
 
Kwa upande wake mgeni maalum katika ufunguzi huo na mwanariadha nguli aliyewahi kuweka rekodi ya aina yake Katika Michezo yya Olimpiki  1968 nchini Mexico, Mzee Stephen John Akhwari amesema kuwa huu ni uwekezaji mzuri uliofanywa na Kampuni ya Multchoice na ni mfano wa kuigwa na wengine.

"Ni kweli kabisa huu ni uwekezaji mkubwa na ni mfano wa kuigwa wa wngine, "amesema Mee Akhwari.

Naye Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday, amesema amefarijika sana na uwekezaji huo wa Multichoce.

Amesema Shirikisho la Riadha la Tanzania litahakikisha kuwa ufadhili huo unakuwa na manufaa na unazaa matunda yaliyotarajiwa ya kuleta medali nyingi zaidi katika mashindano ya kimataifa. “Ufadhili wa aina hii nimuhimu sana kwa maendeleo ya mchezo wa riadha .Tuna ahidi ushirikiano wetu wa dhati ilikufanikisha malengo na tutahakikisha kuwa tunatoa ushikiano unaostahili kwa wafadhili wetu,”amesema Gida.

Mwaka uliopita, kampuni ya MultiChoice Tanzania ilidhamini kambi ya riadha ya timu ya taifa na pia ilimdhamini mwanariadha Alphonce Felix Simbu, ambaye kwa sasa ni miongoni mwawanariadha tegemeo kwa nchi hii. 

Hivi sasa MultiChoice Tanzania inamdhamini mwanariadha kinda Francis Damiano Damasa mbaye ni mshindi wa medali ya shaba katika Micheo ya ya vijana ya Jumuia ya Madola iliyofanyika Bahamas mwaka jana.

Saturday, 15 September 2018

TAA Yawasilisha Tozo ya Huduma za Viwanja Vya Ndege, Kuanza Kutekelezwa Oktoba Mosi 2018


1.   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati) jana akijadili jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara, Bw. Pius Wankali (kulia) na Kaimu Meneja Mipango na Takwimu, Bw. Nasib Elias (mwenye fulana ya bluu bahari) kabla ya mkutano na Wendeshaji wa Mashirika ya ndege kuanza kwenye ukumbi wa Jengo la Pili la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Myerere (JNIA-TB2). Kushoto ni Kaimu Mwanasheria wa TAA, Bw. Elius Mwashiuya.

  Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), jana imewataarifu Waendeshaji wa Mashirika ya ndege za abiria zinazofanya safari zake kuanzia kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) juu ya tozo mpya ya Huduma za Viwanja vya Ndege.

Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela amewaeleza kuwa utekelezaji wa tozo hiyo, ambayo ni dola tano (5) kwa abiria wa nje ya nchi na abiria wa ndani ni Sh. 5,000, utaanza rasmi Oktoba 1, 2018.
Meneja Uwajibikaji wa Shirika la ndege la Safari Plus LTD, Bw. Lauriano Balilemwa jana akitoa mapendekezo kwa ajili ya maboresho ya tozo ya Huduma za Viwanja vya Ndege wakati wa mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Waendeshaji wa mashirika ya ndege zinazofanya safari kuanzia kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Bw. Mayongela amesema lengo la tozo hiyo ni uboreshwaji wa huduma na miundombinu ya Usalama katika Viwanja vya Ndege nchini ili kuhakikisha vinafikia viwango vya ubora vya Kimataifa na pia kutoa huduma bora za kiusalama kwa wadau wake.

Akitoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na ada hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara wa TAA, Bw. Pius Wankali ameeleza kwamba agizo la ukusanywaji wa tozo  hiyo ulitangazwa rasmi na Mamlaka ya Usafiri wa  Anga (TCAA) mwezi Juni mwaka huu.

“Tangazo la kuanzishwa kwa tozo hii lilichapishwa na TCAA kutoka kwenye nyaraka AIC Doc No. TCAA/FRM/ANS/AIS-30, tarehe 29 Juni, 2018 na utekelezaji wake utakuwa ni kuanzia Oktoba Mosi, 2018," amesema Bw. Wankali.

Kwa upande wa wawakilishi wa mashirika ya ndege kubwa kutoka Shirika la ndege Tanzania (ATCL), Bw. Ismail Ismail alitaka kuwepo kwa maelezo ya kina juu ya tozo hiyo, ambayo alitaka ijumuishwe ndani ya tiketi ili abiria awe ameilipia moja kwa moja.

1.   Waendeshaji wa Mashirika ya Ndege zinazofanya safari zake kwa kuanzia kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati mbele) jana alipozungumza nao kuhusiana na tozo ya Huduma ya Viwanja vya Ndege, ambayo itaanza rasmi kutumika Oktoba 1, 2018.

 Kwa upande wake mwakilishi mwingine wa ndege kubwa ya KLM, Bw. Alexander Van de Wint ameomba tozo hii ianze baadaye mwakani kutokana na wao tayari wameshauza tiketi za msimu hadi Desemba 2018 ili wasiwaumize abiria wao.

 Bw. Sammy Ndiramgu (kushoto) jana akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela baada ya kumalizika kwa mkutano na Waendeshaji wa Mashirika ya ndege uliofanyika kwenye ukumbi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Mwenyekiti wa Waendeshaji wa Ndege ndogo za abiria, Chief Uyeka Rumbyambya amesema kuwe na taratibu za kumuhusisha Mkurugenzi Mkuu katika mikutano mbalimbali ya Waendeshaji wa Mashirika ya ndege, ili waweze kuwasilisha.

1.        Naye Kaimu Meneja Mipango na Takwimu wa TAA, ambaye ni mratibu wa mkutano huo, Bw. Nasib Elias alitoa ufafanuzi juu ya ukusanywaji wa tozo hii, ambayo inatarajiwa pia kuwa ni moja ya chanzo cha mapato cha Mamlaka.


1.  Mwenyekiti wa Waendeshaji wa mashirika ya ndege ndogo za abiria, Chief Uyeka Rumbyambya akitoa mapendekezo kwa ajili ya maboresho wakati wa kikao kati ya uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na waendeshaji hao uliofanyika jana kwenye Jengo la Pili la abiria la Julius Nyerere (JNIA-TB II).


Ivan Rakitic Bado Yupo Yupo Sana Barcelona


BARCELONA, Hispania
KIUNGO wa kimataifa wa Croatia, Ivan Rakitic amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain (PSG), lakini amesema hakuna anayeweza kumuondoa Barcelona.

Rakitic haoni hatma yake nje ya Barcelona pamoja na kuwindwa na klabu ya PSG.

PSG wamekuwa wakimuwania kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia, ambaye aling’ara na timu yake ya taifa kwenye fainali za Kombe la Dunia,  lakini Rakitic aliweka wazi kuwa hana mpango wa kuondoka Barcelona.

Rakitic, ambaye alishinda La Liga na mataji matatu ya Ulaya katika msimu wake wa kwanza akiwa na Barcelona mwaka 2015, alitoa mchango mkubwa kwenye kikosi cha kocha Ernest Vervede kushinda taji la La Liga msimu uliopita, anatazamiwa kuwa nahodha ajaye wa timu hiyo kufuatia kuondoka kwa kiungo Andres Iniesta na Javier Mascherano.

"Sioni pakwenda nikiondoka,” alisema Rakitic. “Kuna mada mbalimbali tumezungumza. Nilichukua siku kadhaa kufikiria na kugundua nilipo.

 “Sioni kitu chochote maalumu, najiona nina bahati. Naweza kucheza Barcelona, kuipigania beji hii na hicho kitu kikubwa. Pia mke wangu na mtoto wangu wa kike wanafuraha Barcelona.”

Rakitic  ameanza kwenye mechi zote tatu za La Liga, ambazo Barcelona imeshinda msimu huu na kuiwezesha klabu hiyo  kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.


Benitez Hajutii Kuondoka Kwa Mitrovic


LONDON, England
RAFAEL  Benitez amesisitiza kuwa hajutii kumruhusu mshambuliaji,  Aleksandar Mitrovic  kuondoka kwenye klabu ya  Newcastle United na kutua Fulham.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Serbia mwenye umri wa miaka 23, alijiunga na Fulham kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 27, amefunga mabao sita kwenye mechi tano zilizopita kwenye klabu yake na timu ya taifa, yakiwemo mabao manne kwenye Ligi Kuu ya England.
Kinyume chake, Newcastle imefunga mabao matatu kwenye mechi zake nne za Ligi Kuu ya England, huku kocha Benitez akiziba pengo la mshambuliaji huyo kwa kumleta mshambuliaji Salomon Rondon kwa mkopo wa muda mrefu kutoka West Brom, huku Dwight Gayle akienda upande mwingine na Benitez akimsajili Yoshinori Muto kutoka Mainz kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 9.5.
Kuuzwa kwa  Mitrovic kumeibua maswali kwa mashabiki wa Newcastle, lakini Benitez  haonekani kujutia hilo.
Alipoulizwa kiwango cha  Mitrovic msimu huu Benitez alijibu: "Anafanya vizuri, alifanya vizuri na Serbia, lakini Rondon anafanya vizuri na Venezuela.
"Kila mchezaji ana mazingira yake na anaweza akafanya vizuri kwenye timu moja lakini hasifanye vizuri timu nyingine.
"Tunatakiwa kufanya maamuzi kwa kuangalia kinachohitajika na tulijua nini tunahitaji, hiko hivyo, sasa tunatakiwa kusonga mbele.
"Haitabadili uamuzi wangu. Natakiwa kusonga mbele na Ayoze Perez, Joselu, Yoshinori Mutuo na Rondon, hiko hivyo."

Paul Pogba Amchanganya Mourinho


LONDON, England
KOCHA wa Manchester Uniteds, Jose Mourinho amesema hajui hatma ya kiungo wake nyota, Paul Pogba (Pichani), lakini amejipa moyo na kusisitiza kuwa, kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa bado ataendelea kuwepo katika kikosi hicho.
Hatma ya Pogba  Old Trafford  iko shakani tangu majira ya joto huku kukiwa na uvumi wa kuwindwa na klabu za Barcelona na Juventus.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia alisema mapema mwezi huu kuwa hakuna anayejua kitakachotokea kwa baadae na kocha wa Manchester United Jose Mourinho hana uhakika wa hatma ya kiungo huyo.
Kocha Jose Mourinho.
"Kwa wakati huu niko kizani," alisema Mourinho kuelekea mchezo wa jana dhidi ya Watford.
"Kitu kimoja kiko wazi sana kwangu katika siku zote hizi tuko pamoja hajawahi kuniambia anataka kuondoka.
"Paul  alijiunga na wenzake baada ya Kombe la Dunia wiki moja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu, hivyo tuko pamoja kwa takribani miezi miwili sasa na hajaniambia kama anataka kuondoka au la.”
"Nina uhusiano wa moja kwa moja na wachezaji na hajaniambia kwamba  anataka kuondoka. Kama hajaniambia anataka kuondoka ni kwa sababu anataka kubaki."
Mourinho aliulizwa kama wakala wa Pogba  Mino Raiola  anajaribu kumshawishi kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 kuondoka, alisema hilo ni jambo jipya kwake.

Daraja la Juu Tazara Dar Laanza Kutumika Leo

Daraja la Juu la Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Septemba 15, limeanza kutumika kwa majaribio, ambapo magari yakiwemo madogo na mabasi, yanapita na kupunguza kero ya foleni kwa kiasi kikubwa. Daraja hilo linatarajia kuzinduliwa rasmi mwezi ujao na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Thursday, 13 September 2018

Ndugu wa Mlalamikaji Wakiri Hakuna Wizi JNIA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela aklzungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA) Paul Rwegasha.

Na Mwandishi Wetu
NDUGU wa abiria mmoja (jina limehifadhiwa) wamekiri baada ya kuoneshwa picha za kamera za usalama (CCTV) baada ya  ndugu yao aliyelalamika kwenye mitandao ya Kijamii kuibiwa pochi eneo la mwisho la ukaguzi la abiria wanaosafiri kwenda nje ya nchi,  iliyokuwa na fedha na vitambulisho mbalimbali, wakati akisafiri kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akielekea Dubai.

Bw. Wael Hassan (mdogo wa mlalamikaji), ambaye ni Raia wa Tanzania mwenye asili ya Kiarabu, ametoa kauli hiyo leo kwenye Ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la abiria la JNIA-TB2 katika Mkutano wa Waandishi wa Habari ulioitishwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuhusiana na taarifa hizo za shutuma za wizi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela (katikati) akitoa ufafanuzi leo Jijini Dar es Salaam kuhusu madai ya msafiri mmoja kuibiwa pochi yake katika Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA). Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege nchini, Matanga Mbushi na kulia ni Mkurugenzi wa JNIA, Paul Rwegasha. 

Bw. Hassan anasema ameridhika na picha zote za kuanzia hatua ya kwanza ya ukaguzi na baadaye ukaguzi wa pili, na ameshukuru kwa Mamlaka kutumia fursa hiyo kupiga simu ambayo iliachwa na dada yake, kama moja ya njia ya mawasiliano endapo pochi yake ingepatikana afahamishwe kwenda kuichukua.

“Nimeona matukio yote ile jana nilivyoitwa na hata leo, na hakuna sehemu yeyote nimeona dada yangu ameibiwa pochi ndogo iliyokuwa ndani ya pochi kubwa alilokuwa amelitundika begani muda wote wa safari, maana mimi ndiye nilimsindikiza, lakini yeye (dada) ndio aliyesema ameibiwa sasa sijui ni wapi alipoibiwa ingawa pale checking point ya mwisho ameonekana hata hiyo pochi hajaitoa, ninashukuru sana,” amesema Bw. Wael.
Wael Hassan akikanusha mbele ya waandishi wa habari kuhusu madai yaliyotolewa na dada yake kuibiwa pochi katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Katikati ni Kurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, Richard Mayongela na Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege nchini, Matanga Mbushi.
Hatahivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela amesema hawezi kukataa au kukubali juu ya wizi JNIA unaoripotiwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari kwa kuwa kuna wafanyakazi ambao sio waaminifu, lakini wakibainika wanaondolewa mara moja kulingana na sheria, taratibu na kanuni za kazi na nchi.

“Sisi hatuwezi kukataa juu ya wizi na ndio maana tukasema bado uchunguzi unafanyika na tukaanza kwa kuangalia picha za CCTV na tukaona hakuna wizi wowote pale katika eneo aliposema ameibiwa, lakini bado vyombo vya kiusalama vilivyopo hapa kiwanjani vinaendelea na uchunguzi wa tukio hili, ambalo limeripotiwa kwenye mitandao ya kijamii na kusambaa kwa kasi duniani kote, ,” amesema Bw. Mayongela.
Pia Bw. Mayongela ameshukuru ndugu wa mlalamikaji kutoa ushirikiano kwa kuja na kutoa ushirikiano kwa kukubaliana na picha walizoziona juu ya ujumbe unaodaiwa kusambazwa na dada yao, kwenye mitandao ya kijamii, wakati akisafiri kurudi nyumbani kwake Falme za Kiarabu, baada ya mapumziko mafupi. Kwa mujibu wa Bw. Wael wanaishi maeneo ya Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Hatahivyo, Bw. Mayongela amesema sasa TAA inamkakati kamambe wa kuongeza kamera za Usalama kwenye viwanja vyote, ili kubaini matukio mbalimbali yasiyo ya kiusalama na wizi, na pia wafanyakazi wa Mamlaka na wa taasisi nyingine wanaofanya kazi kwenye viwanja vya ndege wameanza kufanyiwa uchunguzi ili kuwabaini wale wote wasio waaminifu na kuwaondoa mara moja kulingana na sheria, taratibu na kanuni za nchi na ajira.
Bw. Mayongela ametoa wito kwa wananchi na watumia wa viwanja vyote vya ndege nchini, kuhakikisha wanafuata taratibu za kutoa taarifa kwa Afisa Usalama atakayekuwepo kwenye kiwanja husika na kutoa taarifa polisi endapo atakuwa anatatizo linalotakiwa kupatiwa ufumbuzi kabla ya kusafiri, na pia kujikagua kabla ya kufika eneo la kiwanja endapo atakuwa anakitu alichokisahau aidha nyumbani au kwenye gari iliyomleta.
Hatahivyo, kutokana na kadhia hiyo ya kuichafua taswira ya taasisi na nchi kwa ujumla, Bw. Mayongela amesema mlalamikaji anatakiwa kuomba radhi kwa njia ya maandishi na akishindwa kufanya hivyo, hatua zaidi za kisheria zitachukua mkondo wake, ikiwemo ya adhabu ya makosa ya kimtandao.

Kwa upande wa Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Afande Matanga Mbushi amesema kwa mwaka huu, imeripotiwa matukio mawili ya uwizi, na baada ya uchunguzi imebainika hakukuwa na uwizi wowote na baada ya abiria kulalamika amepoteza komputa mpakato na Ipad, na vilipatikana na amepatiwa.

“Huyu abiria wa pili alisema ameacha komputa mpakato eneo la Uhamiaji, lakini baada ya uchunguzi waligundua hakuwa nayo,” amesema Afande RPC Mbushi.

Monday, 10 September 2018

TAA Waanza Kugawa Viwanja Kufidia Wakazi wa Kipunguni Ili Kupisha Upanuzi wa JNIA


Wananchi wakiwa katika ofisi ya mtendaji wakisubiri maelezo kuhusu upimiwaji wa viwanja Mtaa wa Kidole  Kata ya Msongola

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Manispaa ya Ilala, vOfisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Kampuni ya Tanzania Remix imeanza kutekeleza agizo la Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Mhandisi Atashasta Nditiye juu ya ulipaji wa fidia ya viwanja kwa Wananchi wa Kata ya Kipunguni A na Kipunguni Mashariki.

Agizo hilo alilolitoa Agosti 30 mwaka huu, limeanza kutekelezwa leo  kwa Wananchi watokao Kipunguni Mashariki na Kipunguni A kwenda  mtaa wa Kidole na Luhanga kupewa viwanja 537 ndani ya Kata ya Msongola ili kupisha mradi wa upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius  Nyerere (JNIA).


Zoezi la upimaji likiendelea ili kuweza kuonyesha mawe ya upimaji kabla ya kumkabidhi Mwananchi husika mapema leo katika Mtaa wa Kidole kata ya Msongola
Awali, Mhandisi Nditiye alitoa maagizo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege  Bw, Richard Mayongela kushirikiana na Manispaa ya Ilala, Mkuu wa Wilaya na Kampuni ya Tanzania Remix, ambayo ilihusika na upimaji wa maeneo hayo kuhakikisha inawagawia wananchi viwanja hivyo na kuhakikisha viwanja hivyo vina ubora.

“Mshirikiane na Tanzania Remix na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Manispaa  kuwagawia Wananchi viwanja hivi vilevile  shirikianeni na  vyombo vya ulinzi na usalama kuwabaini  wafanyakazi wote wa TAA waliojiingiza kwenye mradi huu na kujipatia viwanja kinyume na utaratibu wakati hawahusiki na mradi huu, wabainishwe na wachukuliwe hatua kali za kisheria,” alisema.

Mmoja wa Wananchi kutoka Kipunguni ambaye ameoneshwa eneo lake akiwa amepiga picha katika eneo hilo  Mtaa wa Kidole kata ya Msongola mapema leo.
Safari Kishiwa na Evaline Malume ni miongoni mwa wananchi walioanza kugawiwa viwanja hivyo na kuishukuru Serikali kutokana na maeneo hayo kuwa katika mazingira mazuri.

Wananchi hao walidai wanawashangaa baadhi ya wananchi wenzao walioathiriwa na mradi huo kukimbilia mahakamani kwasababu mbalimbali  zisizo na mashiko.
"Tuwaombe tu wenzetu wafute kesi waje wachukue viwanja, viwanja hivi vipo kwenye mazingira mazuri tofauti na wanavyofikiri," walisema.

Baadhi ya Wananchi wa Kipunguni Mashariki na Kipunguni A wakiwa na Maofisa wakisubiri kupimiwa maeneo yao katika Mtaa wa Kidole kata ya Msongola mapema leo.
Wapima ardhi Masasu Magenyi (Manispaa ya Ilala) na Hemedi  Fundi  (Tanzania Remix) wakisoma ramani za eneo hilo wakati wa kugawa maeneo hayo kwa Wananchi Mtaa wa Kidole Kata ya Msongola Wilaya ya Ilala mapema leo.