Tuesday, 12 September 2017

Misimamo Ligi ya Mabingwa wa Ulaya 2017-18

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi (kushoto) akiwania mpira na beki wa Juventus, Alex Sandro wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya wa Kundi D kwenye Uwanja wa Camp Nou jijini Barcelona jana usiku.

Kundi A

Nafasi TimuPWDLGFGAGDPts
1Manchester United11003033
2CSKA Moskva11002113
3Benfica100112-10
4Basel100103-30

Kundi B

NafasiTimuPWDLGFGAGDPts
1PSG11005053
2Bayern München11003033
3Anderlecht100103-30
4Celtic100105-50

Kundi C

Nafasi TimuPWDLGFGAGDPts
1Chelsea11006063
2Atlético Madrid10100001
3Roma10100001
4Qarabağ100106-60

Kundi D

Nafasi TimuPWDLGFGAGDPts
1Barcelona11003033
2Sporting CP11003213
3Olympiakos Piraeus100123-10
4Juventus100103-30

Kundi E

Nafasi TimuPWDLGFGAGDPts
1Liverpool00000000
2Maribor00000000
3Sevilla00000000
4Spartak Moskva00000000

Kundi F

Nafasi TimuPWDLGFGAGDPts
1Feyenoord00000000
2Manchester City00000000
3Napoli00000000
4Shakhtar Donetsk00000000

Kundi G

NafasiTimuPWDLGFGAGDPts
1Beşiktaş00000000
2Monaco00000000
3Porto00000000
4RB Leipzig00000000

Kundi H

Nafasi TimuPWDLGFGAGDPts
1APOEL00000000
2Borussia Dortmund00000000
3Real Madrid00000000
4Tottenham Hotspur00000000

Kocha Rodgers akikosoa kikosi chake kwa kichapo

LONDON, England

KOCHA Brendan Rodgers anasema kuwa kikosi chake cha Celtic kilicheza kama vitoto vyenye umri chini ya miaka 12 katika kipindi cha kwanza katika mchezo waliofungwa 5-0 na Paris St-Germain (PSG) wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Mabingwa hao wa Scotland tayari walikuwa nyuma kwa mabao 3-0 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika katika mchezo huo wa ufunguzi wa Kundi B.

Rodgers alisema hakutaka kuwa mkosoaji mkubwa kwa wachezaji wake lakini walicheza vibaya katika kipindi cha kwanza.

"Unatakiwa kuangalia mpira na unatakiwa kukusaidia, kipindi cha kwanza, hatukufanya hivyo, tulicheza kama watoto wenye umri chini ya miaka 12 wakati huo, “alisema Rodgers.

Messi aing'arisha Barca, PSG, Chelsea, United zaua

ZURICH, Uswisi

NYOTA Lionel Messi alifunga mara mbili wakati Barcelona ikipata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Juventus katika moja ya mechi za ufunguzi za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, wakati vigogo vya soka vya Ufaransa Paris Saint-Germain, Manchester United na Chelsea nazo zikishinda kwa kishindo.

Baada ya kipindi kibaya cha majira ya joto, Barca ilikutana na washindi hao wa pili wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu uliopita, kitu ambacho Barcelona ilikuwa haikitaki cha kukutana na wakali hao wa Italia, lakini Messi alikuwa katika kiwango chake bora na kuipatia Catalans pointi zote tatu.

Mchezaji mpya Ousmane Dembele aliyeichezea kwa mara ya kwanza timu hiyo katika Ligi ya mabingwa kwenye Uwanja wa Camp Nou lakini alikuwa Messi ndiye aliyekuwa wa kwanza kufunga bao baada ya kugongeana vizuri na Luis Suarez.

Ulikuwa mchezo mzuri kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina ambao ulisaidia Ivan Rakitic aliyeifanya Barca kupata bao la pili katika dakika ya 56 na Messi aliongeza bao jingine na kuifanya timu hiyo kuwa mbele kwa mabao 3-0 baada ya kufunga bao safi katika kipindi cha pili.

"Mara nyingi nilikuwa matata kwa kucheza dhidi ya Messi na sasa nina bahati kuwa na mchezaji huyo upande wangu, “alisema kocha wa Barcelona Ernesto Valverde.

Matokeo hayo yanaifanya Barcelona kulipa kisasi cha kufungwa na Juventus msimu uliopita baada ya Barca kufungwa katika robo fainali ya mashindano hayo na kuifanya kuongoza Kundi D pamoja na Sporting Lisbon, ambayo ilishinda 3-2 ugenini dhidi ya Olympiakos nchini Ugiriki.

Sporting, ambayo ilikuwa mbele kwa mabao matatu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, itakutana na Barcelona katika mchezo ujao utakaofanyika Ureno.

Wakati Barcelona ikizoea kucheza maisha bila ya Neymar, Mbrazil huyo amekuwa akifurahia maisha na PSG, ambapo alifunga bao la kuongoza wakati timu yake hiyo mpya ikishinda 5-0 dhidi ya Celtic katika mchezo wa Kundi B uliofanyika Glasgow.

Katika mchezo mwingine wa Kundi B, CSKA Moscow ilitoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa wa Ureno Benfica katika mchezo uliofanyika Lisbon, Ureno. CSKA itaikaribisha Man United baadae mwezi huu.

Klabu yazamani ya Mourinho, Chelsea ilipata ushindi mnono usiku huo, baada ya kuisasambua Qarabag 6-0 katika mchezo wa Kundi C uliofanyika kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

 

Mourinho ailaumu Man United licha ya kushinda 3-0

LONDON, England

KOCHA Jose Mourinho ameweka matumaini ya Manchester United kufanya vizuri katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya kuikosoa timu yake `kubweteka’ katika mchezo huo ambao wameshinda 3-0 dhidi ya Basle.

Marouane Fellaini, Romelu Lukaku na Marcus Rashford wote walifunga mabao yao ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya wakati Man United ikishinda kwa urahisi katika mchezo huo dhidi ya timu hiyo ya Uswisi uliofanyika kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Mourinho, anasaka kushinda taji la mashindano hayo kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo akiwa na Porto na Inter Milan, aliwatuhumu wachezaji wake kubweteka baada ya bao la Lukaku lililoifanya timu hiyo kuwa mbele kwa mabao 2-0 muda mfupi baada ya mapumziko baada ya kutawala kipindi cha kwanza.

"Pointi tatu ni muhimu sana wakati unaoanza hatua ya makundi kwenye uwanja wa nyumbani, “alisema Mourinho, ambaye aliiwezesha United kutwaa taji la Ligi ndogo ya Europa msimu uliopita wakati wa shindano lake la kwanza Ulaya tangu aanze kuifundisha timu hiyo msimu uliopita.

"Hadi 2-0 tulikuwa vizuri, tukijiamini na kucheza kwa utulivu, tulifanya maamuzi mazuri, kiujumla tulicheza vizuri.

"Baada ya hapo kila kitu kilibadilika. Tuliacha kufikiri, tuliacha kucheza vizuri, tuliacha kufanya maamuzi sahihi uwanjani na kusababisha kujiweka matatani.”

Basle walipata baadhi ya nafasi nzuri lakini hawakuwa tishio kuwaadhibu Man United katika kipindi cha pili.

Hatahivyo, Mourinho alijua kuwa aina hiyo ya makosa ingeweza kukiadhibu kikosi chake.


Katika mchezo huo Man United walipata pigo baada ya mchezaji wake Paul Pogba, kutolewa nje baada ya kuumia katikati ya kipindi cha kwanza.

Saturday, 9 September 2017

Manchester City yaikandamiza Liverpool 5-0

LONDON, England
MANCHESTER City imetoa kipigo cha `mbwa mwizi’ baada ya kuifunga Liverpool pungufu kwa mabao 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Etihad.

Ushindi huo ni ujumbe mzito wa Manchester City kwenda kwa wapinzani wake wanaoshindana nao kuwania taji hilo la Ligi Kuu.

Liverpool ilipata pigo baada ya mchezaji wake mmoja Sadio Mane kutolewa baada ya kumchezea vibaya hewani Ederson na kusabbaisha kipa huyo kupata matibabu ya muda mrefu kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Claudio Bravo.


Mabao ya Man City yalifungwa na Agüero katika dakika ya 24, Gabriel Jesus katika dakika ya 45 na 53, Sane katika dakika ya 77 na 90.

Katika mechi zingine leo, Arsenal iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya  AFC Bourne huku Chelsea ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Leicester City.

Simba yatoka sare na Azam FC, Yanga leo Njombe

Na Mwandishi Wetu
SIMBA jana imeshindwa kujipigia Azam FC baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex Mbagala jijini Dar es Salaam.

Sare hiyo imeifanya Simba kufikisha pointi nne huku ikitamba na mabao yake saba iliyoyapata katika mchezo wa ufunguzi ilipocheza dhidi ya Ruvu Shooting na kushinda 7-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Prisons ya Mbeya wenyewe walishindwa kutumia vizuri Uwanja wao wa nyumbani wa Kumbukumbu ya Sokoine baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Majimaji 2-1 ya Songea na hivyo kufikisha pointi nne.

Wajelajela hao kama wangeshinda jana wangeweza kuongoza ligi hiyo kwani wangefikisha pointi sita kabla ya mechi za leo, ambapo Mbeya City itakuwa nyumbani dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara, Mtibwa Sugar itacheza dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Manungu.

Mechi zingine kesho ni Singida United itaikaribisha mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Katika mchezo wa jana, Simba ilitawala zaidi kipindi cha kwanza na dakika tatu tangu kuanza kwa mchezo Nicholas Gyan nusura afunge kama sio uimara wa kipa wa Azam Fc Razak Abalora kuokoa.

Dakika ya 18 Azan walilikaribia lango la Simba na kushambulio la nguvu lakini Wnock Agyei nusura afunge lakini alishindwa kutumia vizuri nafasi akliyopata na mpira ukadakwa na kipa Aishi Manula wa Simba.

Mchezaji wazamani wa Azam, John Bocco licha ya kumpiga chenga kipa wa timu hiyo lakini alishindwa kuukwamisha mpira wavuni baada ya kuteleza. 

Vikosi vilikuwa Azam FC; Razak Abalora, Daniel Amoah, Bruce kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohamed, Stephen Kingue, Himid Mao, Salum Abobakar, yahaya Mohamed, Mbaraka Yussuph na Enock Agyei.

Simba; Aishi Manula, Ally Shomary, Erasto Nyoni, Method, Mwanjale, Salim Mbonde, James Kotei, Haruna Niyozima, Mzamiru Yasin, John Bocco, Nicholaus Gyan na Shizza Kichuya.

Wakati huohuo, mabingwa watetezi Yanga leo wanashuka dimbani kucheza na Njombe Mji katika moja ya mechi zitakazopigwa leo.

Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amesema kuwa hawataidharau Njombe Mji lakini wana uhakika wa kuondoka na pointi zote tatu.

Uchukuzi, Takukuru zilivyochuana katika michezo tofauti

Kikosi cha timu ya soka ya Klabu ya Uchukuzi kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi ya kirafiki na Takukuru iliyofanyika kwenye viwanja vya michezo pembezoni mwa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) hivi karibuni, ikiwa ni moja ya maandalizi ya michezo ya Shimiwi iliyokuwa ianze Septemba 15 mkoani Morogoro, lakini imefutwa ili kuelekeza nguvu katika ujenzi wa viwanda. 
 Kikosi cha Takukuru wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya mechi ya kirafiki dhidi ya Uchukuzi walikuwa wakijiandaa na michezo ya Shimiwi iliyokuwa imepangwa kuanza Septemba 15 mkoani Morogoro, lakini sasa imefutwa na wachezaji kutakiwa kuelekeza nguvu kwenye ujenzi wa viwanda.
timu ya Kamba ya wanawake ya Klabu ya Uchukuzi wakivutana na wenzao wa Takukuru katika mchezo wa kirafiki. Uchukuzi ilishinda mivuto 2-0.


timu ya kamba ya wanawake ya Takukuru wakivutana na wenzao wa Uchukuzi katika mchezo wa kirafiki uliokuwa moja ya maandalizi ya michezo ya Shimiwi, iliyokuwa ianze Septemba 15 mkoani Morogoro, lakini imefutwa. 

Timu ya wanaume ya kamba wakivuta na wenzao wa Takukuru katika mchezo wa yaliyokuwa mashindano ya Shimiwi yaliyokuwa yamepangwa kuanza Septemba 15 mkoani Morogoro, lakini yamefutwa kwa lengo la kuelekezwa nguvu katika ujenzi wa Viwanda.


Timu ya wanaume ya Takukuru wakivutana na wenzao wa Uchukuzi katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu wa maandalizi ya yaliyokuwa mashindano ya Shimiwi yaliyokuwa yamepangwa kuanza Septemba 15 lakini yamefutwa ili kuelekeza nguvu kwenye ujenzi wa viwanda.
Mshambuliaji Charles Rungwa wa timu ya Takukuru akiwatoka wachezaji wa Uchukuzi katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na yaliyokuwa mashindano ya Shimiwi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika mkoani Morogoro kuanzia Septemba 15, lakini sasa yamefutwa kwa lengo la wachezaji kuongeza nguvu katika ujenzi wa viwanda. Uchukuzi ilishinda magoli 2-1.  

Friday, 8 September 2017

Kiba kuongoza wasanii kibao Tigo Fiesta 2017

Na Mwandishi Wetu, Arusha
TAMASHA kubwa la muziki la Tigo Fiesta 2017 linazinduliwa rasmi leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa na kushirikisha wanasanii kibao nyota na chipukizi.

Nyota hao wataongozwa na Ali Kiba (pichani), ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha Seduce Me, ambacho kimeipuliwa hivi karibuni na kimepamba vilivyo anga za muziki hapa nchini.

Wapenzi wa muziki watamshuhudia kwa mara ya kwanza Kiba akiimba live kibao hicho, ambacho ni moto wa kuotea mbali.

Baadhi ya wasanii wengine wanaotarajia kufanya vitu vyao katika onesho hilo hilo la leo ni pamoja na Weusi, Darasa, Rostamu, Chege, Dogo Janja, Dogo Aslay, Lulu Diva, Vanessa, Maua, Feza Kessy, Jux, Msaga Sumu, Bright na Jux.

Wasanii wengine ni Ray Vanny, Shishi Baby au Shilole, For Q Ngosha the Don, Madee, Malkia Saida Karoli, Ditto, Christian Bella, Homonize, Foby, Mr Blue na Nandy.


Baadaya Arusha, msimu wa Tigo Fiesta utaelekea Kahama, Musoma, Mwanza, Tabora, Dodoma, Iringa, Songea, Njombe, Sumbawanga,Morogoro, Tabora na mwisho litatua jijini Dar es Salaam Novemba 11.

Liverpool yamuweka kando Coutinho ikiifuata City

LONDON, England
KIUNGO Philippe Coutinho (pichani) ameachwa nje ya kikosi cha Liverpool ambacho kesho kitakwaana na Manchester City katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya England.

Mchezo huo utapigwa mapema kuanzia saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki kwenye dimba la Etihad.

Coutinho, 25, amerejea klabuni baada ya mara mbili akitokea benchi alipoichezea Brazil katika mechi za kufuzu kwa Kombela Dunia 2018.

Mchezaji huyo alikosa mechi za Liverpool za mwanzo wa msimu kutokana na maumivu ya mgongo pamoja na kutaka kuhamia Barcelona.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alisema: "Nimeamua kutomjumuisha katika kikosi changu kitakachocheza na Man City ili aweze kutumia muda kwa ajili ya mazoezi zaidi. Alikubali.”

Klabu hiyo ilitupilia mbali ofa tatu kutoka kwa vigogo vya soka vya Hispania, Barcelona ambao walikuwa wanataka kumsajili Coutinho – aliyeomba uhamisho, ambapo klabu hiyo ilisisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi.

Alifunga katika ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Ecuador Ijumaa ya wiki iliyopita, na pia aliingia kitokea benchi katika mchezo wa Jumanne walipotoka sare ya 1-1 na Colombia.

Mechi zingine leo zitakuwa kati ya Southampton itakayoikaribisha Watford          kwenye Uwanja wa St. Mary's kuanzia saa 11:00 jioni, huku Brighton & Hove Albion ikicheza dhidi ya West Bromwich Albion.

Everton           wenyewe watakuwa wageni wa Tottenham Hotspur katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Goodison Park huku Arsenal  itakuwa na kibarua dhidi ya AFC Bournemouth kwenye Uwanja wa Emirates.

Mabingwa wazamani Leicester City watawakaribisha mabingwa watetezi, Chelsea         kwenye Uwanja wa King Power, huku Stoke City watakuwa wenyeji wa Manchester United.

Thursday, 7 September 2017

Okwi, Murshid watua kuiongezea Simba nguvu


Na Mwandishi Wetu
NYOTA wa kimataifa wa Simba waliokuwa na kikosi cha timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, beki Juuko Murshid na mshambuliaji, Emannuel Okwi wanatarajiwa kutua jana jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC utakaofanyika jesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Akizungmza Waandishi wa Habari kweye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Haji Manara amesema kwamba Juuko na Okwi walitarajia kutua jana na kujiunga na wenzao kambini kwa ajili ya mchezo huo.

“Akina Okwi tunawatarajia kufika leo (jana)  kutoka Uganda na watajiunga moja kwa moja na wenzao kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Azam,” amesema Manara.

Ofisa huyo wa Simba amesema mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu Azam ni timu nzuri na wao wamejipanga vizuri ingawa bado wana majeruhi wawili tu, kipa Said Mohammed ‘Nduda’ na beki Shomari Kapombe.

Manara amesema kwamba Kapombe ataanza mazoezi Jumatatu wakati Nduda ataondoka wikiendi hii kwenda India kwa ajili ya upasuaji wa goti.

Kwa upande wake, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema kwamba kikosi chao kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo na watajitahidi kuvuna pointi tatu ili kuonyesha thamani ya kucheza nyumbani.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu, Simba ni timu nzuri na tunatarajia mchezo utakuwa mgumu, lakini tunaamini pia ubora wa kikosi chetu na maandalizi ni silaha yetu nzuri ya ushindi siku hiyo,”amesema Maganga. 

Mapema katika Mkutano huo, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kwamba mchezo huo utachezeshwa na refa Ludovick Charles wa Tabora, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Abdallah Mkomwa wa Pwani na mezani atakuwepo Josephat Bulali na Kamisaa  atakuwa Ruvu Kiwanga, wote wa Dar es salaam.

Ikumbukwe viingilio katika mchezo huo utakaoanza Saa 1:00 usiku vitakuwa ni Sh. 10,000 kwa jukwaa la VIP na 7,000 kwa mzunguko.

Kibira achukua fomu kutetea kiti chake Chaneta

Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Annie Feith Kibira ni miongoni mwa wadau wa mchezo huo waliojitokeza kuchukua fomu kutaka kutetea au kuwania uongozi wa chama hicho.

Kibira na baadhi ya viongozi wenzake wanaoiongoza Chaneta, walifika katika ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kuchukua fomu kutaka kutetea nafasi zao katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Septemba 30 mjini Dodoma.

Ofisa Michezo wa BMT wa dawati la netiboli, Halima Bushiri amesema kuwa Kibira amechukua fomu kutaka kutetea kiti chake hicho katika uchaguzi ujao.

Bushiri aliwataja wengine waliochukua fomu jana kuwa ni pamoja na kaimu katibu mkuu wa Chanetam, Hilda Mwakatobe anayewania ukatibu msaidizi na ujumbe, Judith Ilunda anayeutaka ukatibu mkuu na ujumbe.

Wengine ni Julieth Mndeme (ujumbe), Mwajuma Kisengo, Asha Sapi, Kilongozi Mohamed.
Bushiri alisema mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Septemba 14 wakati tarehe ya usaili itapangwa na Kamati ya Uchaguzi itakayochaguliwa hivi karibuni.
Aliwataka wadau wa michezo wenye uwezo bila kujali jinsi zao kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu na kuzirejesha kwa wakati ili kuwania uongozi katika chama hicho.


Awali, uchaguzo huo ulipangwa kufanyika mjini Arusha lakini ulihamishiwa Dodoma baada ya kubaini kuwa Chama cha Netiboli Mkoa wa Arusha kilikuwa bado hakijafanya uchaguzi, hivyo kingekosa sifa za kuhudhuria mkutano huo.

Wednesday, 6 September 2017

RATIBA LIGI KUU TANZANIA BARA


Wateja 76 wajinyakulia zawadi kibao DStv

Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo (katikati) akifurahia jambo na Mkaguzi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha Abdallah  Hemed (Kushoto) na afisa wa uhifadhi wateja wa Multichoice Tanzania Erick Mosha  wakati wa  droo ya promosheni ya Jishindie na DStv iliyofanyika leo katika ofisi za Multichoice Tanzania jijini Dar es Salaam. Takriban washindi 200 wamejishindia zawadi mbalimbali kwenye promosheni hiyo ikiwemo safari ya kutalii Zanzibar kwa familia mbili
Na Mwandishi Wetu
WATEJA 76 wa DStv wamejinyakulia zawadi mbalimbali kutoka Multichoice Tanzania katika droo kubwa ya promosheni ya ‘Jishindie na DStv’ ambapo mteja wa DStv anapata fursa ya kujishindia zawadi kwa kulipia king’amuzi chake kwa angalau miezi miwili mfululizo.

Kati ya washindi hao 25 wamejipatia zawadi ya ving’amuzi vya DStv Explora, ambavyo ni ving’amuzi vya kisasa kuliko vyote hapa nchini. Washindi wawili wamejishindia Kifurushi cha Premium cha Tsh 169,000) cha mwezi, wengine wawili Kifurushi cha Compact+ cha Tsh 109 000), huku washindi 10 wakishinda kifurushi cha Compact cha Tsh 69,000), 10 kifurushi cha Famili (39,000) na wengine 25 Kifurushi cha Bomba cha Tsh 19,000.

Washindi wawili wa droo kubwa ambao ni Anicet Macheta wa Kagera na Hassan Juma Hassan wa Dar es Salaam wamejishindia zawadi kubwa kabisa ambayo ni safari ya kutalii visiwani Zanzibar wao pamoja na familia zao zisizozidi watu waNne kila familia.
Meneja Uhifadhi wateja wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo (wa pili kulia) akiongea kwa simu na moja ya washindi wa promosheni ya Jishindie na DStv iliyofanyika katika ofisi za Multichoice Tanzania jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni Abdalla  Hemed  Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania, Ronald Shelukindo (wa pili kushoto) Meneja Operesheni wa Multichoice na Erick Mosha ni wa kitengo cha Uhifadhi wateja Multichoice Tanzania. Takriban washindi 200 wamejishindia zawadi mbalimbali kwenye promosheni hiyo ikiwemo safari ya kutalii Zanzibar kwa familia mbili.
Akizungumza baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo katika ofisi za Multichoiche Tanzania, Meneja wa Uhifadhi Wateja Hilda Nakajumo amebainisha kuwa zaidi ya wateja 30,000 wameshiriki kwenye promosheni hiyo iliyoendelea kwa miezi miwili.

Hilda amesema, wamefurahi kuona kuwa washindi takriban 200 waliopatikana wakati wote wa promosheni wametoka maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo Arusha, Mwanza Dar es Salaam, Kagera, Iringa, Geita Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Ruvuma na mikoa mingine kote nchini.

“Wakati wote DStv tunahakikisha kuwa wateja wetu wanafurahia huduma zetu kwani mbali na kwamba sisi ni vinara katika burudani na michezo, pia tunakuwa na promosheni za mara kwa mara ambapo wateja wetu hupata zawadi mbalimbali” alisema Hilda.

Amesema kuwa mwaka huu ni mwaka wa neema kwa wateja wa DStv kwani mbali na kuongeza chaneli kwenye vifurushi hususani vile vya bei ya chini, pia hivi majuzi DStv ilipunguza bei za vifurushi vyake vyote ili kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata huduma hizo kwa unafuu mkubwa.
Kampuni ya Multichoice Tanzania inayoendesha biashara ya vingamuzi vya DStv, ina umri wa miaka 20 sasa, ambapo ilianza shughuli zake hapa nchini mwaka 1997.