Thursday, 22 December 2016

ukungu wavuruga safari za ndege kwa wanaotaka kwenda kula Krismas sehemu tofauti UingerezaLONDON, England

UKUNGU katika maeneo yote ya kusini mashariki yamevuruga ratiba za ndege kwenye viwanja vya Heathrow, Gatwick na City, imesema Shirika la Ndege la Uingereza la British Airways.

Sintofahamu hiyo jijini hapa iliibuka wakati watu wakisafiri kwa ajili ya kwenda kusheherekea Siku Kuu ya Krismas, ambako walionywa kutarajia mvurugano kuzunguka Uingereza yote wakati kimbunga Barbara kikaribia kutokea.

Ofisa mmoja wa hali ya hewa alisema hali mbaya ya hali ya hewa inatarajiwa kesho Ijumaa na Jumamosi, huku ukungu ukitarajiwa kutokea zaidi katika sehemu za Scotland.

Kumetolewa tahadhari kibao sehemu kubwa ya kaskazini ya Scotland “kujiandaa” kuhusu hali hiyo mbaya ya hali ya hewa.

No comments:

Post a Comment