Saturday, 3 December 2016

Breeeaking news Mzee Yussuf Mzimba afariki dunia
Na Mwandishi wetu
MWANACHAMA mkongwe na muasisi wa Yanga Asili, Mzee Mzimba amefariki dunia, imeelezwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam na kuthibitisha na mtoto wake Ramadhani Kampira, Mzimba alifariki jana na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini.

Hatahivyo, Kampira hakuwa tayari kuzungumza zaidi kuhusu kifo cha baba yake, ambapo alisisitiza kuwa taarifa zaidi atazitoa baadae.

Mzimba atakumbukwa kwa kuendesha harakati za kupiga vikali Yanga kubadilisha kiholela kuwa Kampuni, ambapo aliasisi kundi la Yanga Asili.

Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu Mzee Mzimba. Amina.

No comments:

Post a Comment