Friday, 9 December 2016

Arsenal kuwabakisha Sanchez, Ozil kwa gharama yoyote wako tayari hata kuvunja benkiLONDON, England
ARSENAL imesisitiza kuwa itafanya kila iwezalo kuhakikisha inawabakisha kundini washambuliaji wake muhimu, Alexis Sanchez na Mesut Ozil, anasema kocha wa the  Gunners, Arsene Wenger.

Wachezaji hao amekuwa wakihusishwa na klabu nyingine na, ikiwa imebaki miezi 18 katika mikataba yao, na wako katika mazungumo ya kuongeza mikataba mipya na the Gunners.

"Miezi 18 ni mingi katika soka.  Wachezaji hawa wamebakisha miezi 18 na tunawatarajia zaidi, “alisema Wenger.

"Kwa kweli siamini kabisa kama hilo ni tatizo."

Aliongeza kocha huyo: Mkataba ni kati ya pande mbili na kwa uande wangu nafasi bora ni kufanikiwa hilo mapema.

"Lazima ukubali kuwa makubaliano ni jambo binafsi na siri na watutakiwi kuelezea nini kinachoendelea katika makubaliano yetu.”

Alipoulizwa kama yuko tayari kuvunja utaratibu wa mishahara wa klabu ili kuwabakisha wachezaji hao, Wenger alijibu: "Kama ilivyokawaida tutafanya kila tuwezalo kufanya kile tufanyacho kwa mchezaji mmoja mmoja.”

Sanchez, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Chile amefunga mabao 11 hadi sasa katika Ligi Kuu msimu huu na anaungana na mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa kwa kufunga mabao mengi msimu huu.
Taarifa za magazeti zinasema kuwa mchezaji huyo amekuwa akiwindwa na the Blues na klabu moja ya China.

"Kwanini uende China wakati bado unacheza soka England?” aliuliza Wenger

No comments:

Post a Comment