Thursday, 8 December 2016

Barcelona kuichangia timu ya Brazil wachezaji wake waliokufa katika ajali ya ndege ColombiaBARCELONA, Hispania
KLABU ya Barcelona imeialika klabu ya Brazil ya Chapecoense kucheza nao baada ya kumalizkka msimu huu katika kiindi kijacho cha majira ya joto.

Wachezaji 19 wa Chapecoense na viongozi ni miongoni ma watu 71 aliokufa katika ajali ya ndege wakati timu hiyo ikisafiri kwenda Colombia kucheza mchezo wa kwanza wa fainali ya michuano ya Copa Sudamericana.

Mchezo huo wa kirafiki utakuwa wa taji la Joan Gamper, ambao hufanyika kila mwaka kati ya Barcelona na timu iliyoalikwa.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Barcelona ilisema wanataka kutoa “shukrani”  zao kwa waathirika na kuisaidia klabu ya Chapecoense ili kuibuka upya.

Barcelona imeialika klabu hiyo ya Brazil ya Chapecoense kucheza nao wakati wa maandalizi ya kuanza kwa msimu ujao wa ligi katika kipindi kijacho cha majira ya joto.

No comments:

Post a Comment