Friday 16 October 2015

Yanga, Azam, Simba, Mbeya City hakuna kulala



Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania, Yanga.


Na Mwandishi Wetu
MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara YANGA, mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Simba na Mbeya City ni miongoni mwa timu zitakazoshuka dimbani leo kusaka pointi tatu muhimu.

Yanga watakuwa wenyeji wa Azam FC, ambao katika ligi ya msimu uliopita walimaliza wa pili nyuma ya Yanga, leo wanaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa wakti Simba watakuwa wageni wa Mbeya City katika kipute kitakachofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Pamoja na mechi hizo na zingine za leo, lakini macho na masikio ya wapenzi wa soka yatakuwa kwa Yanga na Azam FC kwani timu hizo kwa sasa ndio zinatawala soka la Bongo.

Mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, unatarajiwa kuwa mkali na wakusisimua, huku ukiamua hatma ya msimamo wa timu hizo mbili, ambazo hazijawahi kufungwa tangu kuanza kwa ligi hiyo.

Tayari timu hizo mbili,ambazo pia ndio washindi wa kwanza na pili katika ligi ya msimu uliopita, kila moja imeshacheza mechi tano na kujikusanyia pointi 15, hivyo endapo moja itapoteza mchezo huo wa leo, itakuwa imeporomoja.

Pamoja na kuwa pointi sawa, lakini Yanga ndio wanaonekana kuwa na safu kali zaidi ya ushambuliaji, kwani wana akiba ya mabao 13 kibindoni wakati wenzao wa Azam FC wamezifumania nyavu mara tisa hadi sasa.
Timu ya Azam FC.
Kwa upande wa mabao ya kufungwa ambayo ndio yanaonesha uimara na ubutu wa beki, Yanga wamefungwa bao moja tu hadi sasa wakati wapinzani wao hao wameruhusu mabao mawili kutinga katika nyavu yao.

Yanga itamkosa kiungo wake mahiri Haruna Niyonzima wakati Azam FC wenyewe watamkosa Jean Baptiste Mugiranez pamoja na Frank Dumayo.

Niyonzima na Mugiranez wako kwao Rwanda ambako walikuwa wakiichezea timu yao ya taifa, lakini Niyonzima pia litumia muda huo kufunga ndoa na wote hawajarudi.

Timu ya taifa ya Rwanda `Amavubi ilicheza dhidi ya Tunisia na Burkina Faso.

Akizungumza Kocha Mkuu wa Azam FC, Stuart Hall alikiri mchezo dhidi ya Yanga kuwa mgumu na kuwakosa Mugireneza na Dumayo, ambaye alifiwa na kaka yake.

Hall alisema kuwa atapanga kikosi chake kutokana na wachezaji aliokuwa nao katika mazoezi na waliofanya vizuri.

Timu hizo zinatarajiwa kuoneshana kazi hasa katika sehemu ya kiungo ambako ndiko mashambulizi na ulinzi utakapoanzia.

Katika mchezo wa hivi  karibuni, Azam FC iliifunga Yanga kwa penati 8-7 baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa.

Shirikisho la Soka Tanzania lilitangaza viingilio,ambapo kiingilio cha chini kitakuwa sh. 5,000 huku kiingilio cha juu kitakuwa ni sh 30,000 kwa VIP A na 20,000 kwa VIP B & C.

Wakati mchezo huo utachezeshwa na Abdallah Kambuzi kutoka mkoani Shinyanga, akisaidiwa na Makame Mdogo (Shinyanga), Robert Luhemeja (Mara), mwamuzi wa akiba Frank Komba (Dar es Salaam), huku Kamishna wa mchezo ni Joseph Mapunda kutoka mkoa wa Ruvuma.

Msimamo:

 Nafasi

TimuMPWDLGFGA+/-Pts

1
Young Africans55001311215

2
Azam550092715

3
Simba SC540173412

4
Mtibwa Sugar540164212

5
Tanzania Prisons631265110

6
Toto African62314319

7
Stand United63034409

8
Mwadui62223218

9
Mgambo JKT622234-18

10
Majimaji621334-17

11
Ndanda512245-15

12
Kagera Sugar612327-55

13
Mbeya City611456-14

14
African Sports510416-53

15
Coastal Union603305-53

16
JKT Ruvu6015110-91

No comments:

Post a Comment